PreGE2025 Sheikh Mkuu BAKWATA Mwanza: Kauli yoyote inayoashiria kuvunja amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu tuikatae

PreGE2025 Sheikh Mkuu BAKWATA Mwanza: Kauli yoyote inayoashiria kuvunja amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu tuikatae

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722


Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke, amesema kuwa kumeanza kutokea viashiria vya lugha mbaya zinazotoka kwa viongozi wa kisiasa nchini, ambazo zinaweza kusababisha amani ya nchi kupotea.

Sheikh Kabeke amesema hayo wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an katika Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika mjini Bariadi, na kushirikisha vijana takriban 30 ambao wamechuana kuhifadhi Qur’an.

Amewataka waumini wa dini hiyo nchini kuwa wa kwanza kukataa kauli hizo na pia kuzilaani, kwani zinaweza kuhatarisha amani ya nchi, ambayo imedumu kwa kipindi kirefu na imewezesha Watanzania kufanya kazi kwa utulivu.
 
Ana maana ile kauli ya Katibu Muenezi wa CCM Amos Makalla?!
 
Back
Top Bottom