Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,764
- 896
Nguruvi3, wewe na Mzee wetu mwenye chama mnapingana matusi ya Lissu kwa Nyerere wewe unayaita data na vithibitisho, msome Mzee Mtei.Tumtake radhi kwani alieleza nini cha maana?
Haya yote yanayozungumzwa sasa tumeyajadili. Labda nikueleza tofauti moja ya Lissu na Mohamed, Lissu anaongea kwa data na vithibitisho. Mohamed Said anaongea kwa hisia 'inasemekana, imesemwa, nilisikia, ati, huenda' n.k.
Nitake radhi upotoshaji,fitna na uzushi, ebo! nidhalilishe uwezo wangu wa kufikiri !
Tadhali nitake radhi kwa kunihusisha na mada za MS
By Edwin Mtei![]()
![]()
Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.
Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.
Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA.
Kazi kweli kweli tutasikia mangi.
Ahsanta.
