Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona disco ndio lanaanza tena.Sheikh Mselem Ali, mmoja kati ya Masheikh wa Uamsho ambao wametoka Gerezani amesema mihadhara yao ilikuwa na nia ya kuwaamsha watu kudai Katiba Mpya.
Amesema kwa kipindi kile walifanya hivyo kwa kuwa kulikuwa na fursa ya maoni kuhusu Katiba Mpya. Walifanya hayo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa katiba in ruhusu kila mtu kutoa mawazio au maoni yake
Aidha amesema hana chama cha siasa, na wala hana mamlaka ya kudai katiba mpya. Lakini ikitokea serikali inataka maoni kuhusu katiba mpya na wakiona anaweza kuchangia mawazo basi atashiriki.
Nakumbuka sana kipindi kile,hadi Jakaya na Dr Shein vichwa viliwauuma sana,naona ndiyo wakaamua kuchukua maamuzi magumu, maana hali ilizidi kua tete kila kukicha kuna tukio jipya,hadi na vile vitoto vya kizungu vilivyoletwa kwa kujitolea eti navyo wakavimwagia tindikali! Watu Wana rohoo ngumu sana!!Watu wanajisahaulisha makusudi kumwagiwa tindikali wageni, kuchomwa moto makanisa wakati wa harakati za uamsho...
Hawakumbuki yule chagga kasisi wa kanisa katoliki alifanywa nini kule Zanzibar nyakati hizo.
Mkuu huu ujasiri hata hao Uamsho kabla hawajakamatwa walikuwa na ujasiri gunia 3,000 kuliko huu.Kawatoa mama au imewatoa mahakama?yeye alichokisema (huyo mama yako) kesi zote zisizojitosheleza kwa ushahidi dpp azifute,na kwa ushauri huo watu wengi walifutiwa kesi zao na hivi sasa wako huru.
Hivi wewe unaamini kwa miaka 9 bado walikuwa wanakusanya ushahidi au walikuwa hawana ushahidi.
Kimsingi hao walikuwa ni wapinzani wa muungano,hawautaki kabisa na ndicho walichokuwa wanawahamasisha wazenji waukatae,ila wenye mamlaka hawakupenda misimamo yao na badala ya kujibu hoja zao,wao wakawafungulia kesi na kwa vile wao wanajiita wanamihadhara ya kiisilamu ikaonekana wakipewa kesi ya ugaidi itaeleweka vizuri zaidi na watu kama wewe ambao kwenu serikali huwa haiongopi.
Acha roho mbayaYaan hao aliowatoa mama kwangu mm naona ni magaidi tuu ata asingewatoa kabsa.
Watu wanapiga tu kelele kwasababu tuko nje ya mfumo.Waache uongo bana, zile clip zao za kusema watamtoa mtu roho mbichi ndio kudai katiba??? Walikua wanaeneza ujinga tu wakawahiwa....