PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Katika taarifa yake kwa wanahabari, Sheikh Saidi Mwaipopo amelaani vikali mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa chama cha CHADEMA, akidai kuwa wanatengeneza taswira ya kuwa wema kwa nje ilhali wana ajenda za siri zisizo za uaminifu.
Sheikh Mwaipopo alieleza kuwa matukio na mikakati ya kisiasa inayofanywa na kikundi hicho inalenga kuondoa serikali halali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuvuruga viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Soma: Sakata la Mhadhiri wa Chuo Kikuu kupewa kesi ya ugaidi, Mgomo wa wafanyakazi UDOM wanukia
Aidha, Sheikh Mwaipopo amewajibu viongozi na wanachama wa CHADEMA wanaoidai serikali inawaonea na kuwasingizia tuhuma za ugaidi wasomi na wahadhiri wa vyuo vikuu waliokamatwa hivi karibuni. Sheikh Mwaipopo amesisitiza kuwa si kweli kwamba serikali inamjulisha au kumsingizia msomi wa chuo kikuu ambaye imemwajiri na kumlipa mshahara, bali vyombo vya ulinzi vinapaswa kuachiwa vifanye kazi yake ya uchunguzi kwa uhuru na kuwatia huru wale watakaobainika hawana hatia.