Sheikh Mwaipopo: Zitto Kabwe una Masters umeshindwa na mtu mmoja mdogo tena standard seven failure

Sheikh Mwaipopo: Zitto Kabwe una Masters umeshindwa na mtu mmoja mdogo tena standard seven failure

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


"Jambo lingine kuonekana kweli wewe ni mtu wa ajabu wa ovyo sana tu. Ungejifikiri tu. Zitto Kabwe uliingia kwenye uchaguzi, wewe una masters, yaani una digrii mbili, umeshindwa na mtu mmoja mdogo, darasa la saba tu, tena standard seven failures.

Darasa la saba Baba Levo amekutoa kamasi, amekutoa jasho, na amekushinda kwa ushindi wa kishindo, alafu kwa aibu na unafiki unaenda kuweka pingamizi mahakamani eti hata niliibiwa. Hivi uliibiwa, kuweka mawakala wa kuhesabu kura zako, haukuweka watu wako kuhesabia kura? Uliweka. Kwa nini unasema umeibiwa? Umeibiwaje? Nani kaiba?

Ni mambo ya uongo, ya kutafuta umaarufu na kutafuta sifa eti uonekane wewe ulikuwa mwanasiasa bora. Uongo Zitto ulishindwa Kigoma hawakutaki. Mimi najua nimekaa Kigoma na pajua Ujiji, wazee wa Ujiji wote nawatafuta. Nawajua, si unaona, nawajua.

Umetawala kule Mwandiga kwa muda wa miaka mitano kama sikosei, au kumi. Kigoma umekaa kama miaka 15. Haki ya Mungu nakwambieni kweli watanzania. Kaa yote ya Zitto Kabwe Kigoma, hakuna lolote alilofanya. Na kama liko alilolifanya atuonyeshe amefanya nini Kigoma Zitto Kabwe.

Mtu aliyefanya kujaribu kuwajenga kidogo watu wa Kigoma ni yule Kigoyogoyo Ngenda, Kilumbe Ngenda. Alivyokuwa mbunge kwa miaka mitano yule bwana alikuwa anakaa Kigoma anasikiliza watu wa Kigoma.

Huyu Baba Levo anaishi, anakwenda Kigoma na anasikiliza kero za watu wa Kigoma. Zitto Kabwe alikuwa anakuja na baibui anaondoka na baibui. Hataki kuomba hata shilingi 100, kwanza mchoyo.

Sasa utakuwa mbunge gani mchoyo? Ni mchoyo Zitto mchoyo. Na ndio maana wakaamua kumpiga chini watu wa Kigoma na sidhani kama utarudi tena bungeni ulijidanganya wakati ule hakuna chochote ulichokifanya bunge la Dodoma, na ni Kigoma. Tuambie umefanya nini? Umewasemea kwa lipi? Zaidi ya fitina na majungu ulikuwa bungeni basi."
 
Zuzu uchambuzi wake wote umejaa ad hominem attacks, badala ya kuangalia track record ya sheria alizozipigania huyo linayemshambulia, linaendelea kuropoka ujinga tu.
 
Sawa Mwaipopo tueleze umeokota ngapi kutoka kwa Clayton (aka BABA LEVO).?
 
Back
Top Bottom