Hili jambo la Lissu liko mahakamani. Kama una mapenzi na Lissu, ungepeleka mawakili pale mahakamani wakaendelea kumtetea. Ungekuwa na akili—na kama kweli watu mna... unajua hii kusoma na kuwa... kusoma kote mnaweza mkasoma lakini akili kuwa bado hamna. Yaani naomba mnisamehe kwa kutumia lugha hii. Unaweza ukasoma sana, wewe una masters, lakini masters yako ya uchumi sioni kama inafanya kazi ya kiuchumi. Inafanya kazi ya kufitanisha watu.
Kwa sababu gani? Wewe ungekuwa mkweli, au una huruma na Lissu, ungewambia Chadema na wewe mwenyewe kwamba:
'Mama Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Amiri Jeshi Mkuu; tunakuomba kwa unyenyekevu, na vyombo vyako vyote vya ulinzi na usalama, na mahakama pia, na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), tunawaomba mumshamehe Tundu Lissu kwa makosa aliyoyafanya.'
Tunaoamba kwa sababu serikali ina ofa, inaweza ikamsamehe mtu yeyote. Inaweza ikamsamehe mtu yeyote aliyekuwa amethibitishwa kuwa ni mhalifu, hata ambaye anahisiwa kuwa ni mhalifu, inaweza ikamsamehe kama amejutia na ametubu.
Sasa mimi nilitegemea utumie lugha hiyo ya kum-plead Rais: 'Tunaoamba Rais wetu, tunaiomba serikali yetu tukufu, tunaoamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visamehe, ametubu.' Na yule mtu aliyeko jela aonyeshe kutubu na kujutia yale aliyoyafanya.
Lakini kwa akili zenu zilivyokuwa za kutafuta umaarufu na sifa, unasema ati: "Tunataka Rais amwachie..." Kwani wewe ulikuwa hujui sheria? Wewe unataka wewe nani? Unamtaka Rais? Rais anatakwa? Rais anaamrishwa? Wewe nani katika nchi hii mpaka umtake Rais?