VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Uamuzi umesomwa muda mchache uliopita hapa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Habari kamili zitafuata. VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar
==========
Sheikh Ponda, Farid wabanwa!
na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemuona Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wana kesi ya kujibu.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Ponda, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), imewasilisha ombi mahakamani la kutaka kubadilisha hati ya mashtaka dhidi ya kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kislamu Zanzibar (JUMIKI) jana.
Sambamba na kuwaona washtakiwa wote walioshtakiwa na Ponda wana kesi, Hakimu Mkazi Victoria Nongwa pia ameamuru kiongozi huyo na wenzake wapande kizimbani na kuanza kujitetea kuanzia kesho na kesho kutwa.
Uamuzi huo ulitolewa jana asubuhi na Hakimu Nongwa ambapo hakimu huyo alianza kuikumbusha mahakama kuwa washtakiwa wote wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa na kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang'ombe Markas.
Sambamba na hilo pia wanadaiwa kujimilikisha kiwanja hicho kwa jinai, wizi wa malighafi zenye thamani ya sh milioni 59 na kosa la tano ni uchochezi ambalo linamkabili Ponda na mshtakiwa wa tano Mukadam Abdallah.
Hakimu Nongwa alisema kabla ya kuanza kuandika uamuzi wake alipitia ushahidi wa 17 na vielelezo 13 vilivyowasilishwa na upande wa jamhuri unaotetewa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka.
Mahakama imeuchambua ushahidi huo na kuona kuna mashahidi ambao ni viongozi wa BAKWATA walitoa ushahidi ulioonyesha kuwa kiwanja cha Chang'ombe Markas zamani kilikuwa ni mali ya BAKWATA lakini ikaamua kubadilishana kiwanja hicho na kampuni ya Agritanza Ltd.
Hakimu Nongwa alisema pia ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri unaonyesha BAKWATA iko chini ya waumini wa dini ya Kiislamu wote nchini, na kwamba kuna baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu hawakuridhishwa na uamuzi wa BAKWATA kuhamishia umiliki wa kiwanja hicho kampuni ya Agritanza Ltd.
Akichambua hoja za wakili wa utetezi, Nassor Juma na Njama, zilizoomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa hawana kesi ya kujibu, alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za migogoro ya ardhi.
Alisema hoja hiyo ya Wakili Nassor anaifananisha mfano ambao baba anayeamua kuuza ardhi halafu wake wanakuwa hawajaridhika na uamuzi huo, watoto wanaweza kwenda kufungua kesi Mahakama ya Ardhi kupinga uamuzi huo wa baba yao.
"Kwa kifupi tu mahakama inasema kesi hii ni ya jinai na ina mamlaka ya kuisikiliza," alisema hakimu.
"Na ieleweke wazi kila kesi ina mazingira yake na kesi hii tunaona kabisa kuna washtakiwa katika maelezo yao ya onyo walikiri kukamatwa katika eneo hilo…sasa mahakama hii imefikia uamuzi kuona upande wa jamhuri umeweza kujenga kesi yao na hivyo imewaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu," alisema Hakimu.
Alisema anaiahirisha kesi hiyo hadi kesho na kesho kutwa ambapo washtakiwa hao wataanza kupanda kizimbani kujitetea.
Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilifunguliwa mahakamani hapo Oktoba 18, mwaka jana, ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano.
Uamsho washtakiwa upya
Ombi la kutaka viongozi hao Jumiki wafunguliwe mashtaka upya limewasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali kutoka ofisi ya DPP, Mohamed Ali Mohammed, na kusababisha kesi hiyo kukwama kuanza kusikilizwa jana mjini Zanzibar.
Alisema kwamba kulingana na ushahidi unaotarajiwa kutolewa katika kesi hiyo kuna umuhimu mkubwa wa hati ya mashtaka ya awali kubadilishwa kwa washtakiwa hao.
"Mheshimiwa tumeamua kubadilisha hati ya mashtaka kulingana na ushahidi wa kesi tuliyokuwa nao," alisema.
Hata hivyo alisema upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika na upande wa mashtaka uko tayari kuleta mashahidi kabla ya kutolewa hukumu ya kesi hiyo.
Hata hivyo maombi hayo ya kubadilisha hati ya mashtaka yalipingwa vikali na mawakili wa upande wa utetezi, Salum Toufiq na Abdalla Juma ‘Kaka'.
Wakili Salum alisema kwamba kesi hiyo imefunguliwa kipindi kirefu bila ya kusikilizwa na kwa mujibu wa sheria inapaswa kufutwa na wateja wake kuachiwa huru.
Alisema kwamba kumbukumbu zinaonyesha wateja wake walifikishwa mahakamani Aprili mwaka jana lakini hadi sasa kesi imekuwa ikichechemea kuanza kusikilizwa na kuchelewesha haki ya kisheria dhidi ya watenja wake.
Upande wake Wakili Abdalla Juma alisema kwamba jambo la kushangaza upande wa serikali unataka kubadilisha hati ya mashtaka wakati mahakama ikiwa imepanga tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Hata hivyo akijibu hoja za mawakili, mwendesha mashtaka katika kesi hiyo, Mohamed Ali, aliipinga hoja ya kutaka kesi kufutwa kwa sababu washtakiwa namba 6 na 7 ndiyo walisababisha kuchelewa kuanza kusikilizwa kesi hiyo baada ya mara mbili kushindwa kufika mahakamni na kushindwa kutolewa ushahidi wa kesi hiyo.
Alisema washtakiwa hao walishindwa kufika mahakamani Desemba 27 na Julai 6 mwaka jana wakati mashahidi wa kesi wakiwa tayari wameitwa kutoa ushahidi wao.
Baada ya Hakimu Khamis Jafari kusikiliza hoja zilizotolewa, alisema kwamba atatoa uamuzi kuhusu hati ya mashtaka kubadilishwa au la leo kabla ya mashahidi kuanza kutoa ushahidi.
Viongozi hao wa Uamsho awali walifunguliwa shtaka kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na sheria no 6 ya mwaka 2004 ya sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Imeelezwa katika kesi hiyo kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Mei 26 mwaka jana, saa 6.30 waliandaa maandamano yasiyo na kibali kuanzia maeneo ya Kinazini, Msikiti, Mabuluu, Michenzani hadi Kwa Biziredi kinyume cha sheria.
Washtakiwa hawa ni Masheikh Farid Hadi Ahmed, Mussa Juma Issa, Mbarouk Saidi Khalfan, Haji Sadifa Haji, Suleman Juma Suleiman, Fikirini Majaliwa, Abdallah Said Ali na Mbarouk Saidi Khalfan na walikana mashtaka hayo.
Source: Tanzania Daima