Sheikh Ponda Issa Ponda amesema hakuna chama cha siasa nchini Tanzania kinachohamasisha vurugu, bali zinaakisi uwepo wa tatizo fulani. Ameeleza kuwa mtu mwenye busara anapobaini dalili za vurugu, anatakiwa kutafuta chanzo cha tatizo hilo ili kusaidia kulitafutia suluhisho.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Hakuna chama kinachohamasisha vurugu, sijaona hata kimoja. [kauli] zinaakisi tatizo, kwahiyo mtu mwenye busara unapoona dalili utatakiwa utafute tatizo ni nini ili utatue hilo tatizo. Sasa wale watu waitwe. Mimi nimemuomba Rais akutane na wadau na vyama vya siasa kuzungumzia haya masuala, hatuwezi kusema tu watu wanavuruga amani."
Ameendelea kusema; "Viongozi wa dini wanachotakiwa kufanya sasa hivi ni kumuomba Rais aite vyama hivi wakae kuangalia hayo makubaliano, hayo madai yakoje, hili jambo likoje, tutapataje ufumbuzi. Hili ndio jambo viongozi wa dini walipaswa kulisimamia kuleta mazungumzo pamoja, sio kiongozi wa dini unasimama afu unapayuka bila kuonesha utafiti wako, yaani kwanini kuna watu wanatamka hayo maneno, kwanini hali hiyo imetokea."
Video: Wasafi TV