Sheikh Ponda Issa: Tuondoe yanayoleta mivutano na chuki ili tufanye maridhiano

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania Tuondoe yanayoleta mivutano na chuki ili tufanye maridhiano. Sheikh Ponda ameyasema hayo katika kipindi cha Kasri kupitia Crown Fm Mei 13, 2026

“Suala la maridhiano ni jambo kubwa sana kitaifa, lakini haliwezi kufikiwa bila kufahamu hali halisi ilivyo. Msingi muhimu unaosisitizwa ni kuwepo kwa utaratibu wa kupata ukweli wa mambo, ndiyo maana sisi tulipendekeza hivyo.

Kwa mfano, mtaendaje kwenye maridhiano wakati bado kuna mambo yanayozalisha chuki kati yenu? Kwa sasa wapo viongozi wakubwa wa vyama vya upinzani walioko gerezani huku mkizungumza kuhusu maridhiano.
Soma Pia: Sheikh Ponda: Tume ya Jaji Chande ilipaswa iseme mauaji ya Oktoba 29 yalikuwa halali au ya jinai

Pia kwa upande wetu sisi Waislamu, kumekuwa na malalamiko ya kesi nyingi za kubambikiziwa, ambapo baadhi ya Masheikh wamehukumiwa kunyongwa.” Sheikh Ponda
 
Serikali sikivu ya CCM inawajibika kufanya mabadiliko makubwa ya kisheria na kuondoa hayo yanayoleta mivutano Ponda, na hatimae tunaelekea kwenye maridhiano ya hiyari🐒
 
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania Tuondoe yanayoleta mivutano na chuki ili tufanye maridhiano. Sheikh Ponda ameyasema hayo katika kipindi cha Kasri kupitia Crown Fm Mei 13, 2026

“Suala la maridhiano ni jambo kubwa sana kitaifa, lakini haliwezi kufikiwa bila kufahamu hali halisi ilivyo. Msingi muhimu unaosisitizwa ni kuwepo kwa utaratibu wa kupata ukweli wa mambo, ndiyo maana sisi tulipendekeza hivyo.

Kwa mfano, mtaendaje kwenye maridhiano wakati bado kuna mambo yanayozalisha chuki kati yenu? Kwa sasa wapo viongozi wakubwa wa vyama vya upinzani walioko gerezani huku mkizungumza kuhusu maridhiano.
Soma Pia: Sheikh Ponda: Tume ya Jaji Chande ilipaswa iseme mauaji ya Oktoba 29 yalikuwa halali au ya jinai

Pia kwa upande wetu sisi Waislamu, kumekuwa na malalamiko ya kesi nyingi za kubambikiziwa, ambapo baadhi ya Masheikh wamehukumiwa kunyongwa.” Sheikh Ponda
Naunga mkono hoja za Sheikh Ponda Issa Ponda.
P
 
Tatizo ni kwamba CCM hawako tayari kwa maridhiano yeyote au mabadiliko. Wanajua kuwa huo ndiyo utakuwa mwisho wao.
Serikali sikivu ya CCM ndio pekee inazungumza habari ya maridhiano gentleman, acha upotoshaji plz 🐒
 
Maneno matupu hayavunji mfupa. Hayo maridhiano wameyaongea kwa miaka 5 sasa.
si kweli,
halafu maridhiano ni mchakato unaohitaji muda wa kutosha wa kujadiliana na sio kongamano au warsha ya siku moja tu gentleman.

ni vema kua wastahilivu na wenye subra wakati mipango na maandalizi ya mazingira ya maridhiano hayo yakiendelea 🐒
 
Si kweli una maana gani? Kwa hiyo zile 4R zilikuwa ni geresha? Au hujui kwe hizo 4R kuna R moja ya maridhiano!
 
Gentleman,
kwani hufahamu kwamba 4R philosophy za Dr Samia Suluhu ndizo zilizorejesha ustawi wa kisiasa na kuifungua nchi miongoni mwa mataifa ya ulimwenguni?

Kwani hufahamu 4R za Dr Samia Suluhu Hassan ndizo zilizowarejesha nchini vibaraka waropokaji wasio na adabu na vibaka wa kisiasa waliokimbilia uhamishoni ughaibuni?

Ina maana kweli hufahamu kwamba 4R philosophy za Dr Samia Suluhu Hassan, ndizo zilizo ondoa zuio na marufuku kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa ikiwa havina muwakilishi eneo husika?

unajizima data au unajisahaulisha makusudi gentleman 🐒
 
ACT alisharidhiana na CCM zamani.
ACT ni sehemu ya SMZ huko Zanzibar.
ACT alikubali kushiriki uchaguzi mkuu, kwasabu alijua atabalansiwa parliamentary seats.
Hata huyo Ado shaibu, ubunge wake ni hisani tu....
Swali ACT anataka kuridhiana mara ngapi? Na nani?
Maridhiano ni usuluhishi baada ya kukosana..kugombana
Unafanye maridhiano na upande ambao hamjagombana?

Mimi nafikiri maridhiano yawe na sura hizi:
1. CCM & NEC vs Chadema
2.Chauma, ACT & others vs Chadema

NB: Kwasabu CCM anaweza kushinikiza vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi vishiriki meza moja ya mazungumzo huku akijua fika vyama hivyo havizungumzi lugha moja, wala havishei malengo ili kuyahujumu hayo maridhiano hayo kwa utaratibu wa kupiga kura ya wengi wape.
 
Back
Top Bottom