Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa wito kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kurejea kumbukumbu za Bunge, ili kuona namna Mbunge wa zamani wa jimbo la Kigoma mjini Zitto Kabwe alivyowasilisha hoja kuhusu uwepo wa matukio ya utekaji na mauwaji nchini, na kuomba Bunge kusimama kwenye nafasi yake katika kuisimamia serikali ili kuhakikisha matukio hayo yanakoma
Sheikh Ponda ameeleza hayo alipofanya mahojiano maalum na Jambo TV hivi karibuni, ambapo amesema amelazimika kutoa indhari hiyo kufuatia majibu ya Spika Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) alipokuwa akijubu kuhusu 'ukimya' wa Bunge kwenye matukio ya aina hiyo.