Mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuongoza wananchi wa jimbo hilo, atahakikisha mfumo wa elimu unapewa uangalizi bora na unafanya kazi vizuri
Akizungumza Oktoba 4,2025 kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Buriaga, Sheikh Ponda alisema kuwa tathmini aliyofanya inaonyesha kuwa Temeke imekuwa ikikabiliwa na matatizo makubwa katika elimu kwa muda mrefu
Aliongeza kuwa madarasa yamejaa wanafunzi wengi sana, jambo linalowafanya walimu kushindwa kufuatilia maendeleo ya kila mwanafunzi ipasavyo
“Kuna upungufu mkubwa wa walimu na madarasa machache, hali inayosababisha elimu kushuka kiwango. Tukipewa nafasi, ACT-Wazalendo itahakikisha kuna walimu wa kutosha na madarasa yanayotosha,” alisema Sheikh Ponda
Ponda pia aliwahimiza wananchi wa Temeke kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura, ili chama chake kipate nafasi ya kuongoza na kutekeleza mipango yake ya kuboresha elimu na huduma nyingine muhimu kwa jamii