Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SHEIKH RAJAB IBRAHIM KIRAMA NA ADHABU YA VIBOKO 1930
Naweka hapa kutoka kitabu, ''Rajab Ibrahim Kirama Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam,'' yale ambayo yamo humo kuhusu adhabu ya viboko:
''Siku ile baada ya kutoka pale Barazani kwa Mangi, Rajabu Kirama akajua kuwa anao watu wanaomuunga mkono katika kutafuta haki.
Hamasa na ghera ya Uislamu ikawa sasa inaenea chini ya Mlima Kilimanjaro.
Lyamungo, Waislamu wakafanya mkutano agenda kuu ikiwa kujenga msikiti na shule ya Waislamu siku zile wakiziita, ''Muslim School.''
Mzee Rajabu sasa akawa anazungumza na watu bila uoga.
Kabla ya kujenga msikiti pale Nkuu walikuwa wanaswali kwenye kijisikiti kidogo cha udongo na kuezekwa kwa nyasi.
Nje ya msikiti huu kulikuwa na mti jina lake '‘Mruka.’'
Muadhini alikuwa anapanda juu ya mti ule ndiyo anaadhini huku chini wako watu wanamlinda asishambuliwe.
Baada ya jaribio lile la kutaka kumuua Mzee Rajabu Waislamu wa Nkuu wakaamua kumpa ulinzi.
Nkuu ikawa imegubikwa na hofu ya chini kwa chini kuwa kuna uwezekano mkubwa pakazuka vurugu kubwa.
Mangi akamshitaki Mzee Rajabu na Waingereza wakamkamata Mzee Rajabu na kumfungulia mashtaka ya kumtukana Mangi.
Kesi ya Mzee Rajabu ilivuma Uchaggani kote na mahakama ilijaa watu kutoka kila sehemu kuja kusikiliza kesi ile.
Ilikuwa haijapata kutokea Mangi kumshitaki raia wake.
Hukumu ikawa Mzee Rajabu apigwe viboko saba kwa kosa la kumtukana Mangi.
Mzee Rajabu akamwambia hakimu kuwa yeye hatokubali kulala chini kuchapwa na mwanamume mwenzake.
Hukumu hii ya viboko ilikusudiwa kumdhalilisha na kushusha hadhi yake mbele ya jamii na wale wote waliokuwa nyuma yake.
Hukumu ilibadilishwa na Mzee Rajabu Ibrahim Kirama akafungwa siku tatu kwa kosa la kumtukana Mangi.
Soma:
www.jamiiforums.com

Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama
KITABU KIPYA: UISLAM ULIVYOINGIA UCHAGGANI Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtoto mdogo wakati Wamishionari wanaingia Kilimanjaro baada ya Mkutano wa Berlin mwaka wa 1884 na Wajerumani wakaingia Uchaggani kuanza kutangaza Injili wakati huo jina alilopewa na baba yake lilikuwa Kirama Mboyo. Baba...