Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Faru...Historia rasmi inayofundishwa Tanzania inatuambia Mwalimu Julius K. Nyerere alikuwa ni mmojawapo wa watu waliokuwa mstari wa mbele kabisa kupambana na ukoloni, na wala hata hiyo historia haitaji dini ya huyo mpambanaji
Nyerere kapata kusema Mkristo alikuwa yeye na John Rupia.
Angalia picha hiyo hapo chini:
Usitishike na historia hii haya yote yanaelezeka wala hapana haja ya kuwabeza wale ambao walisita kuingia katika harakati kwa haraka.
Hizi zote ni changamoto za ukoloni.
Wagawe uwatawale.
Historia rasmi ina makosa makubwa.
Haya makosa ndiyo yaliyonifanya niandike kitabu cha Abdul Sykes (1998).