Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Earle Seaton na Rais Nyerere baada ya uhuru
Kipande cha gazeti hapo chini kinamzunguza Liwali Ahmed Saleh na Sheikh Said Chaurembo aliyekuwa Hakimu Mahkama ya Kariakoo.
1950 Sheikh Said Chaurembo alikuwa katika TAA Political Subcommittee pamoja na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Abdulwahid Sykes, Hamza Kibwana Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, John Rupia na Steven Mhando.
Kamati hii ilijulikana pia kama Constitutional Development Committee ambayo ilipeleka mapendekezo kwa Gavana Edward Francis Twining vipi Tanganyika itawaliwe na mwisho kupewa uhuru wake.
Kamati hii ilidai kwanza pawepo na uchaguzi wa kura moja mtu mmoja na Tanganyika ipewe uhuru baada ya miaka 13.
Serikali ilishtushwa sana na mapendekezo haya na ikaamua kuwaadhibu wale waliokuwa wafanyakazi serikalini. Dr. Kyaruzi akahamishiwa Kingolwira Prison, Hamza Mwapachu akapelekwa Nansio Ukerewe na Abdul Sykes manusra apoteze kazi yake kama Market Master, Kariakoo Market.
Hapa ndipo wazalendo hawa na wao wakaamua sasa ili kupambana na Waingereza mipango ianze ya kuunda chama cha siasa.
Hii ndiyo kamati ndani ya TAA iliyokiongoza chama hiki kuelekea kuunda TANU 1954 na uhuru ukapatika 1961.
Hii document ina sahihi ya hawa wanakamati wote.
Bahati mbaya hii document imepotea na inaaminika imetolewa kwa kunyofolewa katika nyaraka za TANU na katika nyaraka za Tanganyika National Archives (TNA).
Lakini hii document ipo Rhodes House, Oxford, Uingereza. Katika watafiti wa historia ya uhuru wa Tanganyika ni waandishi watatu tu Judith Listowel (The Makingi of Tanganyika, 1965), ndiyo walioigusia katika vitabu vyao, Cranford Pratt (The Critical Phase in
Tanzania, 1976) na mwandishi (The Life and Times of Abdulwahid Sykes...1998).
Hii document ni muhimu sana katika historia ya TAA.
Namaliza kwa kusema kuwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuitayarisha hii document alikuwa Earle Seaton mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa rafiki wa Abdul Sykes.
Hotuba ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955 inatoka katika document hii.