GE2025 Sheikh Shaban Mlewa: Hakuna amani bila haki, na usalama wa uhai

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Shaban Mlewa, amesema hakuna amani ya kweli inapokosekana haki na usalama wa uhai na mali, akisema kuua mtu mmoja ni kuondoa amani kwa jamii nzima.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 22,2025 Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, katika Semina ya Amani iliyokutanisha viongozi wa dini mbalimbali Kanda ya Kaskazini inayoongozwa na kauli mbiu "Kupiga kura ni haki yetu na Amani ya Taifa letu ni wajibu wetu"

“Hakuna amani ya kweli inapokosekana haki na usalama wa uhai na amani, kuwa mtu mmoja ni kuondoa amani kwa jamii nzima” amesema Sheikh Mlewa.

Amesema swala la amani katika Taifa si swala la Serikali pekee, bali ni swala linalohusu jamii yote kwa ujumla, na kwamba amani hujengwa kwa jamii kuwa na tabia ya umoja na utulivu kwa kukemea chuki, uongo Pamoja na kusengenya.

“Raia mwema ndiye anayeleta amani kwa wengine, kuonyesha amani ni kuepuka kila aina ya maudhi, iwe ni ya kimwili au ni ya maneno. Hii inahimiza kujenga Imani na utangamano, baina ya wananchi wote bila kujali tofauti zao za kidini, kikabila au kisiasa” amesema Sheikh Mlewa.

Amesisitiza kwamba kutokana na amani iliyopo nchini kwa sasa, imepelekea Tanzania kuwa Nchi pekee ya kimbilio kwa raia kutoka mataifa mengine, pia kutokana na uwepo wa watu wanaoamini katika uzalendo wa kweli na shirikishi.

Ameongeza kwamba ikiwa kuna mtu yoyote anayetaka kuivuraga amani ya nchi kwa sasa, kuna uwezekano mkubwa mtu huyo akawa na changamoto katika fikra, kwani kutokana na amani iliyopo amesema watanzania wameendelea kuishi pamoja na kushirikiana.

Ingawa ameng'ata na kupuliza,ila angalau huyu tunaweza kumtoa kwenye kundi la mashehe ubwabwa. Angalau amesema kweli japo kweli nusu.

Ukweli unabaki kuwa ukweli;Hakuna amani bila haki.

Wacha watanzania wafanye wanachoona ni sahihi ili kupata kile wanachotaka.

Period.
 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Shaban Mlewa, amesema hakuna amani ya kweli inapokosekana haki na usalama wa uhai na mali, akisema kuua mtu mmoja ni kuondoa amani kwa jamii nzima.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 22,2025 Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, katika Semina ya Amani iliyokutanisha viongozi wa dini mbalimbali Kanda ya Kaskazini inayoongozwa na kauli mbiu "Kupiga kura ni haki yetu na Amani ya Taifa letu ni wajibu wetu"

“Hakuna amani ya kweli inapokosekana haki na usalama wa uhai na amani, kuwa mtu mmoja ni kuondoa amani kwa jamii nzima” amesema Sheikh Mlewa.

Amesema swala la amani katika Taifa si swala la Serikali pekee, bali ni swala linalohusu jamii yote kwa ujumla, na kwamba amani hujengwa kwa jamii kuwa na tabia ya umoja na utulivu kwa kukemea chuki, uongo Pamoja na kusengenya.

“Raia mwema ndiye anayeleta amani kwa wengine, kuonyesha amani ni kuepuka kila aina ya maudhi, iwe ni ya kimwili au ni ya maneno. Hii inahimiza kujenga Imani na utangamano, baina ya wananchi wote bila kujali tofauti zao za kidini, kikabila au kisiasa” amesema Sheikh Mlewa.

Amesisitiza kwamba kutokana na amani iliyopo nchini kwa sasa, imepelekea Tanzania kuwa Nchi pekee ya kimbilio kwa raia kutoka mataifa mengine, pia kutokana na uwepo wa watu wanaoamini katika uzalendo wa kweli na shirikishi.

Ameongeza kwamba ikiwa kuna mtu yoyote anayetaka kuivuraga amani ya nchi kwa sasa, kuna uwezekano mkubwa mtu huyo akawa na changamoto katika fikra, kwani kutokana na amani iliyopo amesema watanzania wameendelea kuishi pamoja na kushirikiana.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Shaban Mlewa, amesema hakuna amani ya kweli inapokosekana haki na usalama wa uhai na mali, akisema kuua mtu mmoja ni kuondoa amani kwa jamii nzima.
 
Kuhubiri amani, huku haki za msingi za raia zikipuuzwa, ni upumbavu tu.
 
Back
Top Bottom