Sheikh Sharifu Mikidadi alikosa kosa kumchoma mtu kisu utotoni Mimi Deo Kisandu nikampanchi

Sheikh Sharifu Mikidadi alikosa kosa kumchoma mtu kisu utotoni Mimi Deo Kisandu nikampanchi

Humjui kabisa huyo jamaa. Kiufupi huyo ni tapeli tu wala hajawahi kiwa sharifu, jina lake ni msopa. Acha uongo wewe
Haaa, upo right 2009 alianza kupokea mihadhara kama mwenyej wao hasa uwanja Wa bahressa manzese ghafla namuona kwenye TV kawa Sharif, kweli vyuma vimekaza
 
*UTABIRI WA HALI YA NDOA*
Wanaume watakuwa wakali kipindi cha January mpaka mwanzoni mwa february na kwa wanawake walioolewa na watumishi wa umma kutakuwa na vipindi virefu vya hasira na kusonya
Aidha ukanda wa ```Michepuko``` hali haitakuwa shwari kwa sababu PESA hazitavuma kutoka mifukoni mwa wanaume. Kiwango cha juu cha ```usaliti``` kitapungua na kufikia 0. 75% wakati chuki ndani ya ndoa ikiongezeka kufuatia uhaba wa pesa.
Utabiri huu wa hali ya ndoa umeletwa kwenu na ```Mamlaka ya hali ya Ndoa nchini```
AHSANTE
Siku njema.
 
Sijaona sehem uliopanchi aseeh, au kujikunja chenyewe ndo we umepanchi? U got serious problem mzee, wahi kwa Dr bado ukiwa unajitambua. Maana unapoendea utaanza vua nguo adharani ukashindwa jielezea kwa Dr
 
Deo Kisandu wewe kiboko. Sasa ni wapi ulipompanchi huyo Sherifu Majini? Nimeusoma uzi wako wote hakuna mahali ulipoelezea jinsi ulivyompanchi Sherifu Majini ili asimchome kisu Atanasi.

Kaazi kweli kweli.
 
Mzee wa kuwekewa kitu kigumu kama nyoka matakoni umeamka tena? Wewe ni noma.
 
View attachment 668330 Kipindi cha mwaka 1988 Bwana Sharifu Mikidadi Matongo aliletwa Mtaani kwetu Kilima, nyihogo hapa wilayani Kahama, akitokea Shinyanga. Alifikia kwa MAMA HINDU, Wakati huo wote tulikuwa watoto wadogo.

Sharifu Mikidadi Matongo kipindi hicho alikuwa anavuma sana kama Malaika wa Mungu anayetenda miujiza akiwa mtoto, basi watu wengi wenye imani ya Kiislaam walimlaki sana. Alipofikia kwa MAMA HINDU ambapo baba yangu alikuwa amemwoa mtoto wa Mama Hindu Bi.Tausi (mama wa kufikia), nakumbuka Sharifu Majini alikaa karibia mwezi mzima kahama hapo kwa Mama Hindu akitembelewa na kutembezwa maeneo mbalimbali wilayani Kahama. Kalikuwa kanajidai sana, Mimi kalikuwa kana nikera mpaka basi.

Ilikuwa ikifika wakati wa kucheza Sharifu alikuwa hataki tuvae kaputula au Bukuta kwa mujibu wa imani ya Kiislaamu. Mimi siku moja nikavaa kaputula aliponiona akakasirika kweli akanishitaki kwa Bibi Mama Hindu ili nipigwe lakini alimwambia muache tu. Alikuwa ananiogopa sana huyu dogo utotoni.

Basi siku ingine akaja mtoto wa baba wa kufikia Atanasi amevaa kaputula, Sharifu alipomuona alipaniki sana na alikuwa amevaa kanzu, basi akaingiza mkono mfukoni akatoa Kisu vile vidogo vya kukunja ili amchome kwa kuvaa kaputula, Sharifu akanyanyua Kisu kumchoma Atanas ile anafikisha mwilini mwa Atanas kikajikunja na kumwachia maumivu mwenyewe. Hahahahaha nilicheka sana siku hio.

Mmoja wetu akamtania mbona MASHAKA(yaani Deo Kisandu) akivaa kaputula unamwogopa, Sharifu alikaa kimya akiwa na hasira Kisu kimemuumiza mwenyewe. Wakati huo Atanas amekwisha kimbia.

Kimsingi nimemkumbuka Yesu wa Islam Sheikh Sharifu ambaye mtaa mzima alipoondoka alituacha akiwa ametumwagia Majini, wengine wakawa Vibaka wengine Vichaa wengine maisha yao yakaharibika, Mimi nikapelekwa kijijini. Yaani nikikumbuka huyu mgeni wetu wa utotoni na vunjaga mbavu sana.

Imaani ya Kiislaam lazima iangalie uvumilivu wa kuvumiliana na imani na mitazamo ya dini zingine ili tusichomane visu kisa swala la imani.

Deogratius Nalimi Kisandu.
4 January 2018.

IYO picha uliyoweka wewe huyo ni shehe sharifu originally, ,,,Yule Taperi ni mweupe
 
Back
Top Bottom