Sheikh Sharifu Mikidadi alikosa kosa kumchoma mtu kisu utotoni Mimi Deo Kisandu nikampanchi

Sheikh Sharifu Mikidadi alikosa kosa kumchoma mtu kisu utotoni Mimi Deo Kisandu nikampanchi

Ahahahha, huyu jamaa ni kituko sana, kama dish la startimes kipind cha mvua
Nimegundua mwezi ukiandama au ukikaribia kuandama. Katika Jamii Forum kunakuwa na Threads nyingi sana. Hii inaonyesha kuna na viwango vya machizi fresh
 
Sijelewa umedhamiria kusema nini

Sharif majini chief msopa kada wa chama cha mapinduzi

Sharif mikidadi matongo au sheikh Sharif

Hawa si rejea katika uislam

Usijifunze dini hii kwa kuwatazama watu bali uko msingi wa dini hii nayo ni Quran
 
View attachment 668330 Kipindi cha mwaka 1988 Bwana Sharifu Mikidadi Matongo aliletwa Mtaani kwetu Kilima, nyihogo hapa wilayani Kahama, akitokea Shinyanga. Alifikia kwa MAMA HINDU, Wakati huo wote tulikuwa watoto wadogo.

Sharifu Mikidadi Matongo kipindi hicho alikuwa anavuma sana kama Malaika wa Mungu anayetenda miujiza akiwa mtoto, basi watu wengi wenye imani ya Kiislaam walimlaki sana. Alipofikia kwa MAMA HINDU ambapo baba yangu alikuwa amemwoa mtoto wa Mama Hindu Bi.Tausi (mama wa kufikia), nakumbuka Sharifu Majini alikaa karibia mwezi mzima kahama hapo kwa Mama Hindu akitembelewa na kutembezwa maeneo mbalimbali wilayani Kahama. Kalikuwa kanajidai sana, Mimi kalikuwa kana nikera mpaka basi.

Ilikuwa ikifika wakati wa kucheza Sharifu alikuwa hataki tuvae kaputula au Bukuta kwa mujibu wa imani ya Kiislaamu. Mimi siku moja nikavaa kaputula aliponiona akakasirika kweli akanishitaki kwa Bibi Mama Hindu ili nipigwe lakini alimwambia muache tu. Alikuwa ananiogopa sana huyu dogo utotoni.

Basi siku ingine akaja mtoto wa baba wa kufikia Atanasi amevaa kaputula, Sharifu alipomuona alipaniki sana na alikuwa amevaa kanzu, basi akaingiza mkono mfukoni akatoa Kisu vile vidogo vya kukunja ili amchome kwa kuvaa kaputula, Sharifu akanyanyua Kisu kumchoma Atanas ile anafikisha mwilini mwa Atanas kikajikunja na kumwachia maumivu mwenyewe. Hahahahaha nilicheka sana siku hio.

Mmoja wetu akamtania mbona MASHAKA(yaani Deo Kisandu) akivaa kaputula unamwogopa, Sharifu alikaa kimya akiwa na hasira Kisu kimemuumiza mwenyewe. Wakati huo Atanas amekwisha kimbia.

Kimsingi nimemkumbuka Yesu wa Islam Sheikh Sharifu ambaye mtaa mzima alipoondoka alituacha akiwa ametumwagia Majini, wengine wakawa Vibaka wengine Vichaa wengine maisha yao yakaharibika, Mimi nikapelekwa kijijini. Yaani nikikumbuka huyu mgeni wetu wa utotoni na vunjaga mbavu sana.

Imaani ya Kiislaam lazima iangalie uvumilivu wa kuvumiliana na imani na mitazamo ya dini zingine ili tusichomane visu kisa swala la imani.

Deogratius Nalimi Kisandu.
4 January 2018.


Kwahiyo unasema ulitupiwa majini na Sheikh Sharif ndio maana dish limecheza?
 
Yaani uneleta mada kiuhanjaujanja ili isifutwe. Tumekushitukia..
 
Back
Top Bottom