Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Nimesoma hiyo habari ya Mzee Haidar Mwinyimvua imenigusa sana. Kuna watu walijitolea sana kuchangia ukombozi na uhuru.
Hata miaka ya baadae mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa, kuna watu walijitolea sana kujenga vyama wakiamini vingeleta mabadiliko waliyotamani, ambayo naweza kufananisha na wale waliodai uhuru zamani. Nimeona wafanyabiashara waliojitolea majengo yao yakawa ofisi za vyama, nimeona waliotoa magari yao, wapo walioacha kazi zao wakatumikia vyama mfano majuzi niliona interview ya Prof Safari akieleza alivyoacha kazi chuo cha diplomasia na akakosa kazi ya nje ya nchi kwa sababu ya kutumikia vyama vya upinzani.
Kwa bahati mbaya waliopambana na CCM wengi wao wameishia kupata hasara tu. Lakini hata ndani ya CCM yenyewe kuna watu wametumia rasilimali zao kuwezesha kundi fulani wanalolipenda lipate ushindi, wale wa makundi yaliyoshindwa walipata hasara, na hata katika wale walioshinda kuna wengine walikuja kukosana kwa sababu mbalimbali nao wakapata hasara pia. Hivi kwa kutazama zile kampeni za 2015 jinsi Nape alivyokuwa akimpambania JPM, nani alitarajia kuwa Nape angekuja kuadhiriwa hadharani na kuaibishwa? Siasa ni mchezo mchafu tangu zamani.