Sheikh yahya atua Dar

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
434
Mutabiri maarufu sheikh yahaya Hussein aliyekuwa amezushiwa kifo amewasili leo asubuhi saa tatu na ndege la shirika la Ndebe la kenya (kenya airway)akitokea nchini india kwa matibabu
Sheikh yahya anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari leo alasiri
 
Mimi nilidhani ilikuwa "april fool" kumbe watu wabaya wa roho za watu eh! sisi wengine tunaomba mafisadi wafe kabla 2010, lakini wa mungu kama hawa wabakie kutupa habari njema, si tabia nzuri kusema mambo yasiyo na hakika. long live shekh.
 

sasa na wale wanaokwenda kwake kwa matibabu anawapa ujumbe gani? kwani hakuna waganga wa kumtibu hadi aende hospitali India?
 
Pole Sheikh, lakini hapa kuna somo muhimu pia. Ilikuwaje sheikh na utaalamu wake wooote alishindwa kujua kuwa atazuliwa kufa!? Anawezaje kutabiri ya wenzake tuu!
 
Pole Sheikh, lakini hapa kuna somo muhimu pia. Ilikuwaje sheikh na utaalamu wake wooote alishindwa kujua kuwa atazuliwa kufa!? Anawezaje kutabiri ya wenzake tuu!

Mganga hajigangi!
 
alipotua kadai kuwa JK alimpa dola 10,000 za matibabu

MENGI kampa dola 5,000

KUNA MTU MWINGINE NISHASAHAU JINA KAMPA DOLA 1,000

akatibiwe India

TYPICAL SHEIKH ATTENTION WHO*RE atuachii nafasi tukapumua
 
Huyu naye ana mgongano wa maslahi ingawaje kafanya vizuri kuyataja. Hizo pesa JK za kwake au katoa kwenye fuko letu? Zingeweza kuokoa wagonjwa wengi sana Muhimbili badala ya kuwapatia wachache kwenda kutanua nje huku walalahoi wanakufa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…