Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Ali Kadogo, ameibuka upya katika siasa baada ya awali kutangaza kupumzika. safari hii, ameonekana kwenye kikao maalum cha chama cha CHAUMMA, akitoa kauli kali iliyowagusa wengi, hasa walioko kwenye vyama vya upinzani.
Kadogo amesema kuwa mapambano ya kisiasa hayawezi kufanyika kwenye mitandao ya kijamii bali uwanjani, akisisitiza kuwa vita inapiganwa eneo la vita.
Soma, Pia: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Shekh Ally Mohamed (Kadogoo) ajivua Uanachama
Akionekana mwenye huzuni kuhusu mabadiliko ndani ya CHADEMA, Kadogo ameeleza kuwa chama hicho kimepoteza misingi yake ya awali. Amesema kuwa badala ya majadiliano na kusikilizana, sasa baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakitishiana, ambapo mtu akiamua kuondoka, anaambiwa aondoke zake bila kupewa nafasi
Ingawa hakutangaza rasmi kujiunga na CHAUMMA, Kadogo ameonesha kuunga mkono harakati za chama hicho na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zake, jambo linalozua maswali kuhusu mwelekeo wake mpya kisiasa.
Hatua hii inaibua mjadala mpana, huku wengi wakijiuliza kama Kadogo atatangaza rasmi kujiunga na CHAUMMA na kuanza ukurasa mpya wa harakati
Chanzo: JAMBO TV