Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Odemba: Wanaohimiza sana uwepo wa amani kuliko haki ni kama pale ambapo... Wewe kwako, kati ya amani na haki, kipi ambacho kinapaswa kutangulia zaidi?
Mataka: Amani inatakiwa iwepo ili haki iweze kushamiri, ipi ambayo inapaswa kupewa kipaumbele zaidi? Wataalamu wameyejadili sana hayo, kipi kitangulie baina ya amani na haki? Lakini wengi wanasema amani kwanza itangulie, ili haki iweze kusimamishwa? Wewe unasemaje?
Bila shaka amani kwanza. Amani kwanza, amani kwanza. Kwa sababu haki ni jambo mtambuka, linahitaji pia kuzungumzwa na kupeana, linahitaji pia kujadiliwa. Ni lazima mkae chini, hamwezi kukaa chini wakati wa mapambano na vita.
Odemba: Unadhani ya kwamba amani inaweza ikapatikana pale ambapo haki haipo?
Odemba: Ni kweli. Amani inaweza kupatikana hata bila haki?
Mataka: Amani bila ya haki, amani bila ya haki, hiyo itakuwa ni amani ya udanganyifu, lakini inaweza ikapatikana. Lakini amani inatakiwa itangulizwe ili ile haki iweze kuimarishwa. Haki, haki ni jambo lililojadiliwa ili kila mwenye haki aweze kupata haki yake. Lakini inahitaji mazingira ya kuweza kuijadili hiyo haki na kupeana haki.
Odemba: Hivyo amani kwanza kwako? Amani kwanza ndipo haki ije?
Mataka: Amani kwanza lazima iwepo amani ili hiyo haki iweze kushamiri