Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wewe una akili na busara sana. Hizi dini zilitukuta na zitatuacha. Waletao udini wanasumbuliwa na ugonjwa uitwao apodomia au unyani na arabism au uarabu.Waislamu na Wakristo katika nchi hii ya Tanzania udugu wao ni wa kale; mapenzi baina yao ni ya muda mrefu, na hata ushirikiano wao umejengwa katika misingi ya amani na heshima kwa vizazi vingi.
Qur’an Takatifu inatukumbusha: ‘Na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja, na sisi ni wenye kunyenyekea Kwake’ (Qur’an 29:46). Hii ni damu ya udugu, msingi wa umoja, na chemchemi ya taifa letu lenye upendo.