Shellukindo na Kamati Yako Mmepatwa na Nini?

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,972
Maelezo haya hapa chini yanayohusu Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imenisikitisha sana kwa jinsi Kamati hiyo ilivyotishiwa nyau na mambo ya "Posho Mbili kwa kazi moja!"
Source: Mwananchi

Mimi sioni, kwa kauli za Shellukindo kama tuna wapambanaji katika vita hii ya ufisadi! Mjadala wa Richmond ndio huo umezikwa rasmi jana, wapambanaji (ukimwondoa Dk Wilbrod Slaa na Christopher ole Sendeka) wanaonekana walinywea kama wamenyeshewa mvua maskini! Hata hivyo nimefurahishwa sana na jinsi Dk Wilbrod Slaa alivyopambana mpaka mwisho! Soma kauli yake hapa chini:

SOURCE: Mwananchi

Hongera sana Dk Wilbrod Slaa! Upambanaji wako utakumbukwa daima na Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu!
 
Uliona hata Speaker Sitta alivyouongoza mjadala huu? Tuachane na mawazo finyu kwamba kuna badiliko lolote la maana linaweza kuletwa na Bunge letu hasa baada ya vikao vya NEC ya CCM kutoa angalizo kwa Sitta.
 
hii nchi chi imekwisha.
watu walianza kwa kasi sana
mwisho wa siku jambo limeisha ki aina,
 
Hivi huwa mnategemea kabisa kuwe na mabadiliko yeyote??? CCM is for life...I LOVE CCM!!!...Mtaandika ,mtalalamika....mitego yote iko makini...
 
CCM ni wanafiki sana mie siwapendi hawa watu, wanabadirika kama kinyonga, hawapo pale kwa ajili yetu wapo kwa maslahi yao na yale matumbo yao tuuu. tunajidanganya sana kwa kuwategemea hawa watu ilhali wao ni wanachama wa chama hichochicho cha mafisadi, bila sisi wananchi wa kawaida kuzinduka hakuna cha maana kitafanyika nchii hii
 


Watu pipoooooooo. CCM si wanafiki ila watu ndio wanafiki kwani unakumbuka ya Dr. H. Mwakyembe? ni CCM hiyo lakini unajua unafiki upo kwa hao Mafisadi si CCM. CCM safi Kikwete safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii spika safi?
 
Kwa mwendo huu, kamwe CCM haiwezi kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Maslahi ya watu binafsi au chama hayapaswi kuzidi yale ya Taifa. Viongozi wetu wanadhani maslahi ya CCM ndio ya Taifa! Shame!
 
Mafisadi tunaomba muwashughulikie wapambanaji wote wa ufisadi kwa kuwa wametudhalilisha kulko. Mwageni fedha za kutosha wakose ubunge kwa kuwa ni wanafiki wa kutupa.
 
Wapiganaji wa ufisadi CCM wanapigania nini? Sishangai unafiki ulioonyeshwa na shelukindo/mwakyembe/sitta/manyenye/sendeka/kilimba/mpendazoe katika kuhitimisha suala la RICHMOND..

Nasikitika sehemu kubwa ya jamii bado haijawaelewaa vemaa wanafiki hawa wa demokrasia nchini. kwa hili natumai adhabu yao INAKUJAAA...
 
naona hapa akina shelukindo wamesalimu amri kwa maslahi ya chama chao ccm. kama kawaida watanzania ni waoga na wala hatuna amani ya kweli. hawa jamaa wametishiwa sana mpaka umefika wakati wameona heri wabwage manyanga kuliko kuendelea kukwaruzana na watawala. kwa mtaji huu maendeleo ya nchi hii tutaendelea kuyasikia kwenye radio tu na kamwe hatuta endelea. huu ndio ulikuwa muda muafaka wa kuwa wajibisha viongozi wabovu kwa masalahi ya taifa. natamani jeshi lichukue madaraka ya nchi kwa muda kidodgo lisafishe uozo wote and then viongozi wa kiraia warusidhiwe nchi baada ya kansa ya uongozi mbaya kuondoka. excessive democracy imeproove failure especially kwa nchi zetu za kiafrika.
 
Wapendwa wangu wanaJF, tusiwalaumu wapambanaji wa mafisadi wamejitahidi kadri walivyoweza ila wamekosa 'support' na ifahamike kuwa 'system' iliyopo sasa ni vigumu kwa mtu yeyote awaye yote kujipambambanua dhidi ya mafisadi maana 'system' itself is created by UFISADI, Hivyo hata ungekuwa wewe mwanaJF ungepambana weee lakini mwishowe unajikuta upo peke yako. Kinachotakiwa hapa ni Mapinduzi ya fikra (mindset) na mtazamo wa wananchi wenyewe chini ya mwamvuli 'People's Power'. Otherwise, nothing will change in this country.......
 

Nchi hii sijui tumuamini nani sasa?
 
Crime doesn't pay. Tutaendelea kufunika funika uovu mpaka lini?

My prayers are that God will give us more Willibrod Slaas so that Tanzania can be salvaged after 2010.
 
Nchi hii sijui tumuamini nani sasa?

Hakuna! Ni vyema uchukulie hivyo uondokane na huzuni. CCM imefanikiwa sana katika kujenga mfumo wa kifisadi kiasi kwamba anayejaribu kuutikisa hapati uungaji mkono wa dhati - hata toka kwa wananchi wenyewe. Wala hakuna haja kuwalaumu wabunge (kamati, wapiganaji, n.k.) kwa kushindwa kuidhibiti Serikali.

Ni yule aliye tayari kujitoa mhanga ndiye anayeweza kwenda kinyume na "msimamo" wa Chama. Na usishangae wa-TZ kwa ujumla wao wakimuona mjinga tu. Kuhusu ukombozi wa kifikra sidhani kama ni tatizo hapa. Watu wanaujua ufisadi vizuri sana hadi vijijini lakini umeshakuwa sehemu ya maisha yao. Ukitaka kupambana na mfumo huo kwa dhati kabisa (badala ya kisiasa) basi uwe tayari kukosana hata na baadhi ya ndugu.

Mimi huwa naota siku ambayo wananchi watapunguza ushindi wa CCM katika Bunge na Serikali za mitaa ANGALAU kwa robo tu ndipo nikubali kwamba sasa wa-Tanzania wanahitaji mabadiliko - wanatuma ujumbe maalumu kwa viongozi. Lakini kila uchaguzi ni ushindi wa kishindo! Hapo tena mbunge gani awe na ujasiri wa kupingana na Chama kikiamua kushikilia msimamo wake?
 
Dr. Mwakyembe na Selelii wamesema nini kwenye huo mjadala hapo jana?

Mwakyembe na Selelii wote wamekalia makuti makavu majimboni watokako pamoja na Mpendazoe, kwahiyo ndio maana wamekubali yaishe pengine mafisadi watawaonea huruma warudi mjengoni!! Kulikuwa hakuna sababu ya kusalimu amri dakika za mwisho kama ni kuogopa kuenguliwa na ccm wakati wa uchaguzi, kuna falling back position ya kuwa Independent; hawana sababu ya msingi ya kuthrow in the towel!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…