Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Maelezo haya hapa chini yanayohusu Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imenisikitisha sana kwa jinsi Kamati hiyo ilivyotishiwa nyau na mambo ya "Posho Mbili kwa kazi moja!"
Mimi sioni, kwa kauli za Shellukindo kama tuna wapambanaji katika vita hii ya ufisadi! Mjadala wa Richmond ndio huo umezikwa rasmi jana, wapambanaji (ukimwondoa Dk Wilbrod Slaa na Christopher ole Sendeka) wanaonekana walinywea kama wamenyeshewa mvua maskini! Hata hivyo nimefurahishwa sana na jinsi Dk Wilbrod Slaa alivyopambana mpaka mwisho! Soma kauli yake hapa chini:
Hongera sana Dk Wilbrod Slaa! Upambanaji wako utakumbukwa daima na Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu!
Source: MwananchiAwali, Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini, ilionekana kumgwaya Dk Hoseah kwa kushindwa hata kuhoji kwanini mamlaka ya juu (Rais) imeshindwa kumwajibisha katika hilo.
Taarifa hiyo iliweka bayana kwamba, kamati imeamua kumwacha DK Hoseah mikononi mwa mamlaka ya juu tofauti na maneno yake ambayo alikuwa akiyatoa nyuma na hata yale yaliyotolewa na kamati hiyo katika mkutano wa 16.
Akizungumzia kwanini wameamua kutotaka kujadili tena azimio namba tisa kuhusu Dk Hoseah, alisema ni kwa sababu ya uchunguzi ambao umekuwa ukifanywa na Takukuru dhidi ya wabunge.
"Kamati yangu haikuweza kulizungumzia hili kwa sababu mkurugenzi wa Takukuru ameanzisha zoezi la kuwachunguza wabunge. Kamati imeona haitakuwa haki kutolea maelezo au majibu kwa serikali kuhusu azimio hili," alisema Shellukindo.
Mimi sioni, kwa kauli za Shellukindo kama tuna wapambanaji katika vita hii ya ufisadi! Mjadala wa Richmond ndio huo umezikwa rasmi jana, wapambanaji (ukimwondoa Dk Wilbrod Slaa na Christopher ole Sendeka) wanaonekana walinywea kama wamenyeshewa mvua maskini! Hata hivyo nimefurahishwa sana na jinsi Dk Wilbrod Slaa alivyopambana mpaka mwisho! Soma kauli yake hapa chini:
SOURCE: MwananchiKwa mujibu wa Dk Slaa, hakuelewa mantiki ya kukosekana majina ya watu muhimu waliopaswa kuwajibishwa kama aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini (Arthur Mwakapugi), kuachiwa hadi wanastaafu na wengine kutowajibishwa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mbunge huyo wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chadema, alihoji pia mantiki ya Kamati ya Nishati na Madini kumwacha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk Edward Hoseah, kwa sababu nyepesi ya uchunguzi wa posho mbili unaofanywa na taasisi hiyo dhidi ya wabunge.
"Kuna mambo mengi ya msingi humu kwenye ripoti hayamo, kumwacha Hoseah kisa eti anafanya uchunguzi wa posho mbili dhidi ya wabunge ni jambo ambalo halina maana, kwa sababu hivi ni vitu viwili tofauti kabisa," alifafanua Dk Slaa.
"Kama ni uchunguzi wao kuhusu posho mbili waendelee na yeye kama ni kuwajibishwa hilo ni jambo jingine, kuliacha jambo hili katika mamlaka ya juu wakati Bunge ni chombo chenye nguvu na kushusha heshima ya Bunge."
Dk Slaa aliongeza kwamba, :"Uchunguzi wao waendelee kama mimi nimekula posho mbili wanichunguze waje wanikamate, lakini kuogopa uchunguzi wa Takukuru kuna walakini, nilikwishasema uchunguzi wa Takukuru usije ukafunga watu midomo."
Katika kuonyesha msisitizo, Dk Slaa aliweka bayana kwamba Dk Hoseah alionywa kwa kutokuwa makini na kutaka serikali ifafanue kama kosa hilo adhabu yake ya mwisho ni onyo au vinginevyo.
Mbunge huyo ambaye amejizolea sifa kutokana na kupambana na ufisadi, alihoji pia serikali kujaribu kusafisha hata wajumbe watano wa Timu ya Mashauriano ya Mikataba Serikalini (GNT), wakati walikuwa ni sehemu ya ushauri katika mkataba huo ambao uliitia serikali hasara.
Hongera sana Dk Wilbrod Slaa! Upambanaji wako utakumbukwa daima na Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu!