Shem darling Jackie na bro wangu Reggie wamempoteza Dangote

Shem darling Jackie na bro wangu Reggie wamempoteza Dangote

Tee Bag

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
7,220
Reaction score
5,622
SHEM DARLING JACKIE NA BRO'ANGU REGGIE WAMEMPOTEZA DANGOTE

BASI bwana! Kwenye public domain kwa miaka kadhaa sasa, mtoto wa mama Nasibu, Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ndie alikuwa mtawala wa mapicha ya malovee na wapenzi wake.

Alishafunika mbaya na Wema, akang'arisha na Penny, akanyoosha na Zari, juzijuzi mapichapicha na Tanasha yalikong'oli kunako internet domain. Ile mipicha ilifanya wadada wamuone Dangote ni gentleman malaika. Wakasema: Diamond anajua kucare!

Si unajua dogo Dangote na shoo zake? Mara kabeba gauni la Wema lisiburuze chini. Halafu anaonekana anamvalisha viatu Tanasha. Anamfungulia mlango wa gari Zari. Very protective young man kwa akina mamsapu wake. Na haya ndo mambo wanawake wanapenda. Wanapenda kuonekana malkia.

Shoo za Dangote kwa wapenzi wake zilifanya wadada wamtolee mfano kuwa mwanaume bora kimapenzi. Habari za Dangote kubadili wapanzi mara kwa mara hazikuwakera. Wao walisuuzika kumoyo na ule ugentleman wake wa kwenye kamera.

Nilimsikia ndugu yangu mmoja anashushuliwa na mkewe: "Hivi wewe yule mtoto mdogo Diamond anakushinda nini? Humuoni anavyomfanyia Zari, mpaka mwanamke unajiona malkia. Hutaki na mimi nijione malkia?" Dah! Dogo wa Tandale alileta mushkeli ndani ya familia za watu.

Siku hizi unadhani Dangote ana nyimbo basi? Tena baada ya kumnanga Mobeto kuwa ni mchawi, wanamwogooopaa! Wanawake hawapendi wanaume wenye kudhalilisha wanawake. Couple ya moto mjini ni bro'angu Reggie wa Aipiipii na shem darling Jackie.

Mtandao wameushika aisee! Mapichapicha ya mahabati. Siku hizi wanaume tunaambiwa: "Hamna hela na mahaba hamjui. Mengi ana pesa na mahaba anayajua." Kimsingi bro'angu Reggie na shem darling Jackie wamemfunika Dangote, ila kwetu tabu ipo palepale. Wanaume tunatakiwa tuwe na hela, halafu tutoe good times kwa akina mamsapu kama Reggie kwa Jackie.

Ile ile video ya anniversary, bro'angu Reggie sijui alipata ugonjwa wa kutetemeka? Maneno sikuyasikia vizuri. Bro Reggie aliongea kama Edo wa Monduli. Ati nini? Reggie na Jackie wapo kileleni! Reggie na Jackie ndo Couple ya Taifa.

Ndimi Luqman MALOTO

FB_IMG_1554213323228.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nlchojfunza unaweza waona wanacheka kumbe ndani balaa wala mambo ya mtandaoni sio ya kahadaikia kabsaaa
Unaeza kuta mzee show hapig vzur na mdada anataka show off mbele za watu afanyeje
Haya mambo ni kutulia na yako
Watu wanatuigizia mnoo mpka wanatuchanganya cc ambao bado kuolewa ![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom