Ndugu, naomba urudie kusoma upya. Nimesema alianza mwaka jana kununua na kuvaa nguo hizo.
Ukiw na tabia ya kuvunja ndoa za watu, unaweza kufanya kama unavyofikiri.
Pia nakuomba ufahamu kuwa suala hili tunalichukulia not as a very delicate but also a fragile issue.
unaposema 'tunalichukulia' wewe na nani mnaolichukulia?
Anapovaa mumewe si anamuona?
Kama anamuachia toka chumbani ujue anapenda mkewe avae hivyo.....
Huyo mke wa kaka yako ndo yao na maisha yao hayakuhusu..... Ingekuhusu pale tu kaka mtu angekuja kukuomba ushauri lakini sio wewe umshauri.....
Gari la familia, familia ya nani? Mlichanga kama familia kununua au ni gari la kaka yako ndo unaliita la familia? Kama ni hivyo ndo maana unadhani kuwa una mamlaka juu ya mapaja ya mke wa kaka yako.....
Unajuaje kama kaka yako anapenda kuona mapah!ja ya mkewe kwenye gari? Ila nyie 'familia' ndo mnaingilia privacy yao?
Kma unaishi kwa nduguyo nakushauri uondoke uende kujitafutia pako, uachane na mapaja ya shemejio......
Ndoa ina mambo mengi sana, sio kila jambo kaka yako akwambie, na kama mkewe kaanza kuvaa ghafla, unajuaje landa kaka yako kamwambia anapenda? Ila kwa vile 'ndugu' mnadhani mna mamlaka ya kutoa mawazo yenu inabidi afunike funike?
Unajua shemeji yako na mkewe wakiwa chumbani wanaongea nini?
Duniani watu hawatafuti uadui, epuka mifarakano isiyo na msingi...... Shemeji yako anaweza kukugeuzia kibao kwa ndugu yako wewe ukaonekana adui......
Ndo maana unaambiwa mambo ya ndoa waachie wanandoa wenyewe........... Mke anavaa anapanda kwenye gari mume wala hana habari hujui kuwa anapenda?
Shaurilo.....
Ukiambiwa umevunja ndoa ya watu ndo utakuja kuelewa kuwa ya ngoswe muachie ngoswe.....
Kumguka mke wa kaka yako, hakuhusu, unless umeshirikishwa, usijishirikishe..... SHaurilo