Kingsmen
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 279
- 213
Poleni na majukumu wataalam, naombeni msaada kidogo katika hili jambo...
Miaka ya nyuma kidogo au naweza nikasema ni late 80`s nilifanikiwa kukabidhiwa ardhi na baba angu mkwe ambae mimi nilioa binti yake wa pili kwa kuzaliwa. Kutokana na ukaribu wetu mimi na mkwe wangu akaamua kunikabidhi ardhi mimi na mume mwenzangu aliyeoa binti yake wa kwanza.
Huyu mzee alifariki mwanzoni mwa miaka ya 90 hivyo wenzetu wengine waliooa baada ya kufariki hawakuweza kupata hiyo bahati.
sasa huyu mume mwenzangu yeye aliuzaga ardhi yake muda mrefu sana ila mimi sio mtu wa tamaa na ukizingatia naishi mbali kidogo hivyo kule kijijini nimefanya kama sehemu ya kuzalisha tu.
sasa juzi mke wangu alienda kwao kidogo kuwatembelea ndipo ndugu zake wakamueka mtu kati na kumueleza kuwa wamepanga kufungua kesi ili nipokonywe ardhi niliyopewa na baba mkwe kwa hiyari yake..
Na ambaye ame initiate hiyo sikomoko ni shemeji yangu anaefuata baada ya kuzaliwa mke wangu. Maana ndie mtoto wa kiume yeye alizaliwa middle 70`s .
sasa nilikua naomba maelekezo kwa wanaofahamu vizuri sheria katika jambo kama hili mlolongo wake upoje..
Mimi sitaki ugomvi na hii familia, na sihitaji kutumia nguvu kubwa kuendesha kesi nahitaji sheria ifuate mkondo na kama ikihitajika nguvu basi naweza pia kufanya hivyo..
Nawasilisha.