Mimi ndio huwa napingana sana na watu, kwa sababu ni mwanao eti hata akiwa na tabia mbaya unaona sawa tu cause ni mwanao? huko sio kumpenda bali kumpotosha. Lazima mumuonyeshe kwamba tabia yake si nzuri na haikubaliki kwa Mungu na katika jamii nzima. Kama anataka kushirikiana nanyi basi aache hiyo tabia.
Mimi nina binti mmoja tu, na sijui kama nitakuja pata mtoto mwingine ila kwenye masuala ya malezi niko makini sana sijali eti kwa sababu yuko pekee basi kila afanyacho ni sawa, akikosea namuadabisha vizuri tu bila kujali yuko pekee au la, kifupi sina mchezo kabisa. Huwa anashangaa sometimes ila nadhani akija kua mkubwa ndio ataelewa nilikuwa namaanisha nini.