Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
SHEMSA MOHAMED: CCM TUPO SIMIYU KUHAKIKISHA SERIKALI INATEKELEZA MAJUKUMU KWA WAKATI
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali kutoka Mkoa wa Simiyu, tarehe 4 Juni 2025 wamefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Busega kwa lengo la kusikiliza, kushughulikia na kutatua kero za wananchi.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Shamsa Mohamed, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenan L. Kihongosi. Ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo na inaendeshwa kwa karibu baina ya Chama na Serikali.
Katika mikutano na wanachi na vikao na viongozi wa Wilaya, Wananchi walieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo hali ya miundombinu ya barabara, uhaba wa maji safi, changamoto katika sekta ya afya na elimu, pamoja na upatikanaji wa pembejeo za kilimo.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Chama, Ndg. Shamsa Mohamed alisema kuwa CCM itaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi katika kuhakikisha huduma bora zinapatikana na maendeleo yanawafikia wote.
"Tumesikiliza kwa makini kero zenu. CCM tupo hapa kuhakikisha Serikali inawajibika na inatekeleza majukumu yake kwa wakati. Tunasimamia haki, maendeleo, na utu wa Mtanzania. Kazi kubwa bado ipo, lakini kwa mshikamano wetu—tunasonga mbele" Ndg. Shamsa.
Viongozi wa Serikali waliopokea maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti walielekezwa kufuatilia na kutekeleza haraka maazimio ya ziara hiyo kwa kushirikiana na wananchi.
Kazi na Utu, Tunasonga