Pre GE2025 Shemsa Mohammed Ahamasisha WanaCCM Kujiandikisha Daftari la Wapiga Kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amewaagiza viongozi wa Matawi, Kata na Mashina kuhamasisha wanachama kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili wapate sifa za kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kuimarisha Chama na kukagua uhai wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Mwandoya wilayani Meatu akiwa kwenye ziara ya Tarafa kwa Tarafa.

Shemsa amesema ili wana CCM wapate haki ya kuchaguliwa na kuchagua viongozi wanaowataka lazima wajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura.

"Tunaelekea kwenye uchaguzi wa wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025, twendeni tukahamashishe wana CCM na wananchi wenye sifa wajiandikishe katika daftari la wapiga kura ili wawe na sifa" - Shemsa Mohammed

"Tujiandikishe ili kukipigia kura Chama Chama Mapinduzi (CCM), ushindi wa vijiji na vitongoji unategemea tutakavyojitokeza kujiandikisha" - Shemsa Mohammed

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Shemsa Mohammed amesema wanajipanga kupitisha wagombea wanaokubalika, waadilifu na wanaotimiza wajibu wao kwa wanachi.

MWISHO.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…