Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Ndugu Shemsa Seif Mohammed amewataka Wabunge na Madiwani kuhakikisha wanatekeleza ahadi zao binafsi walizotoa kwa wananchi wakati wanaomba kura kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
Mwenyekiti Ndugu Shemsa Seif Mohammed amewataka ametoa wito huo kwenye ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa katika Tarafa ya Nyalanja kata ya Mwamanongu wilayani Meatu wakati akiongea na viongozi wa kata, mabalozi na viongozi wa dini.
Ziara hiyo inayolenga kuimarisha uhai wa Chama pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi huku akiwasisitiza viongozi wa kuchaguliwa kutimiza ahadi zao.
"Niwatake viongozi wa kuchaguliwa na wananchi, timizeni ahadi zenu binafsi kab la hatujafika kwenye uchaguzi mkuu 2025…tekelezeni ahadi zenu, msipotekeleza tutapata kazi wakati kuomba kura" - Ndugu Shemsa Seif Mohammed amewataka