TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Shehena ya kemikali hatarishi aina ya salfa imemwagika katika barabara kuu ya Morogoro-Iringa, karibu na eneo la Mindu Mikoroshini, baada ya lori lililokuwa likiisafirisha kupata ajali.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo limezua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, kutokana na ukaribu wa mahali hapo na Bwawa la Mindu ambalo maji yake hutumika kwa zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro.
Mwandishi wetu, Theresia Mwanga, aliyefika eneo la tukio, ameripoti kuwa juhudi za kuondoa kemikali hiyo tayari zimeanza.
Wananchi wa eneo hilo wameeleza wasiwasi mkubwa wakihofia athari za kiafya na kimazingira, huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na madhubuti kabla kemikali hiyo haijafika kwenye maji ya Bwawa la Mindu.
Hadi sasa, juhudi za kuzipata mamlaka husika ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo bado zinaendelea.