Shenena ya Kemikali hatarishi yamwagika barabara kuu ya Mikumi jirani na bwawa la Mindu

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Shehena ya kemikali hatarishi aina ya salfa imemwagika katika barabara kuu ya Morogoro-Iringa, karibu na eneo la Mindu Mikoroshini, baada ya lori lililokuwa likiisafirisha kupata ajali.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo limezua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, kutokana na ukaribu wa mahali hapo na Bwawa la Mindu ambalo maji yake hutumika kwa zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

Mwandishi wetu, Theresia Mwanga, aliyefika eneo la tukio, ameripoti kuwa juhudi za kuondoa kemikali hiyo tayari zimeanza.

Wananchi wa eneo hilo wameeleza wasiwasi mkubwa wakihofia athari za kiafya na kimazingira, huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na madhubuti kabla kemikali hiyo haijafika kwenye maji ya Bwawa la Mindu.

Hadi sasa, juhudi za kuzipata mamlaka husika ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo bado zinaendelea.

 
Bila shaka wewe utakuwa unatokea kwenye hilo bwawa ndo maana umetoka kuja kulalamika
 
Hizo kemikali hatari mbona zinaonekana zilibebwa kizembe sana! Kwa nini hzikuwekwa kwenye container?
Naona hapo kuna uzembe mkubwa na kutofuata sheria. Huyo mwenye hilo gari lazima atatozwa faini ya kutosha.
 
Hiyo Sulfur itakua ilikua inaenda kutengenezea mbolea zikina Ammonia Sulfate. Kusema kwamba ilikua inaenda kutenenezea sulfuric acid possible ila rahisi kutwngeneza Dar nakusafirisha product.

Hafu Imebebwa kifala sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…