Sherehe kubwa Lumumba, CHADEMA wakiparurana

Sherehe kubwa Lumumba, CHADEMA wakiparurana

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Misahafu inasema mwana mpotevu aliporudi kwa babaye, mwana mwema aliyekuwa kabakia Kwa babaye alichukia mno. Kwamba kwanini baba yao amfanyie sherehe mwovu huyo hali yeye alikuwa pale siku zote asifanyiwe dhifa yoyote?

"Kwa hasira kali alisusa sherehe ya nduguye, akaondoka nyumbani na kutokomea kusikojulikana na asirudi tena, milele."

Karudi Slaa. Hoja zake tunaziona. Tunawaona kina Mwabukusi na wa namna hIyo, wakiongea lugha za watu tulizokuwa tumezikosa mno.

"Kulikoni Chadema uchwara kuungana na ma CCM kuudhika au hata kudhamiria kuwakwamisha au kutaka kuufisha mwamko huu mpya?"

Kwamba machadema uchwara hayo yameuvaa u CCM kuicheza ngoma hIyo kwa uzuri zaidi?

Kwamba hii sasa ni kwa niaba ya ma CCM, siyo?

"Kwa hakika patakuwa pana sherehe kubwa sana pale Lumumba!"
 
Vita ya panzi furaha ya kunguru

Mtafaruku huu utatonyesha mengi.

Wacha mvua inyeshe tuwajue wenzenu mapandikizi walioko huku.

Agenda za wananchi ni kipaumbele. Si ruzuku Wala ubunge.
 
Unamzungumzia yule padri mzinifu aliyesema lissu alipigwa risasi na cdm au?

Ninazungumza mwana mpotevu aliyerudi kwa baba yake.

Pia namgusia yule mwema aliyesusa Kwa kuwa nduguye karudi.

Wewe waona mwenye nafuu ni yupi?
 
Sisi tunagonga kaulanzi tu 😂😂

Gongeni vilauri ndugu wakati tunasafisha nyumba yetu. Hatoki mtu. Tutabanana hapa hapa!

#Wenye nchi wananchi
#wenye chama wanachama
#Tutaelewana tu.
 
Ninazungumza mwana mpotevu aliyerudi kwa baba yake.

Pia namgusia yule mwema aliyesusa Kwa kuwa nduguye karudi.

Wewe waona mwenye nafuu ni yupi?
Samahi bro Mimi nilikuwa nje ya mada kwasababu nilikuwa nawazia kile kizee kilichotemwa ubalozi Sasa kameanza kujitia kizalendo ni kazee Fulani kalichoasi upadri na chama mwaka 2015 samahani sana mkuu
 
Back
Top Bottom