Sherehe ya ushindi wa Azerbaijan

Sherehe ya ushindi wa Azerbaijan

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Wananchi wa Azerbaijan wametoka mitaani kusherehekea ushindi dhidi ya uvamizi wa Armenia Nagorno-Karabakh na kutiwa saini kwa makubaliano.

Raia wa Azerbaijan walianza kufurika barabarani baada ya Rais İlham Aliyev kutoa hotuba kwa umma.

Mji mkuu wa Baku ulienea shangwe na sherehe za ushindi. Maelfu ya wakaazi wa Baku walisherehekea ushindi huo kwa kubeba bendera za Azerbaijan na Uturuki.

Baadhi ya wananchi wa Azerbaijan walisherehekea ushindi huo kwa kucheza mziki huku wengine wao wakizungukwa kwa magari barabarani.

Kwa uzalendo walioonyesha mioyoni mwao, wananchi hao walitokwa na machozi walipokuwa wakiimba wimbo wa taifa na nyimbo za asili ya Kituruki.

Wakaazi wa mji wa Ganje ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo pia walisherehekea ushindi wa kukomboa maeneo kutokana na uvamizi wa Armenia.

Mamia ya raia wa Azerbaijan walikusanyika katika eneo la wazi la Azadlık wakiwa wamebeba bendera za Azerbaijan na Uturuki.

Wananchi hao walitoa kaulimbiu za "Mashahidi hawafi, nchi haigawanyiki", "Askari wakubwa ni askari wetu", "Karabakh ni yetu na itabaki kuwa yetu" na "Simama Imara mama wa mashahidi", na baadaye wakaandamana pamoja kwenda kwenye sehemu ya ukumbusho ya Heydar Aliyev.

Sherehe za wananchi zikaendelea hapo.
 
Wanasherehekea nini sasa wakati wakazi wa eneo hilo ni Wakristo na hawataki kutawaliwa na Azerbaijan?
 
Back
Top Bottom