Sherehe za kuzima mwenge Tanga - Live

Mkuu, shukrani sana. Errors nimejitahidi kurekebisha accordingly.

Kaondoka na gari lake jipya? Naona State House wamebadili wanatumia X5 cars siku hizi. Linafanana hivi?

..Mkuu najaribu kupekua pekua nijue price range ya huu mtambo....Nadhani muungwana nae amekuja na style mpya ya usafiri anaotaka kutumia......Bado kuna shule Kigoma wanafunzi wanakaa sakafuni hakuna madawati wao wanatukoga tu na migari yao.....
 
Na jukwaa lilikuwa hivi:

Hawa jamaa chini walikuwepo!

Pia hali ilikuwa hivi:
 
Mzee Mwanakiji,

Hapo ni ushahidi wa kisyansi au research? Maana ushahidi wa kisayansi utaupata vipi kwenye hilo?

Ushahidi wa kisayansi unafuata kanuni za kisayansi:

a. Unapima watu wanaoshiriki katika kukimbiza mwenge kabla hawajashiriki mbio hizo kujua hali zao za HIV

b. Unawalinganisha na kundi jingine ambalo linakuwa ni control group

c. unafuatilia kundi hilo la wanaoshiriki mbio za mwenge na lile lisiloshiriki mbio za mwenge

d. Unapima baada ya muda fulani kuona ni lipi limeambukizwa zaidi au la

e. Unarudia majaribio hayo hadi uwe na sample ya kutosha kuweza kusema kuwa angalau kuna uhusiano (correlation) kati ya kukimbiza mwenge na kuongezeka maambuziko ya HIV kwenye kundi fulani kulinganisha na control group.

that is how you would do it in a nutshell..
 
..Mkuu najaribu kupekua pekua nijue price range ya huu mtambo....Nadhani muungwana nae amekuja na style mpya ya usafiri anaotaka kutumia......Bado kuna shule Kigoma wanafunzi wanakaa sakafuni hakuna madawati wao wanatukoga tu na migari yao.....

Angalia usije ukapata price ya yale tunayoyaona mitaani, haya yana special featues, hasa za usalama, kwa ajili ya ulinzi wa viongozi, kwanza nadhani ni bullet proof. Kwa hiyo hata bei zake zitrakuwa tofauti na haya tunayotanua nayo mitaani
 
Mkuu Mkjj, huko vijijini mwenge ukilala watu ndo wanapata nafasi ya kuambukizana, wanaoambukiza si wale wakimbiza mwenge, ni wanavijiji wenyewe kwa wenyewe wakitumia mkesha wa mwenge as an excuse
 
Mkuu Mkjj, huko vijijini mwenge ukilala watu ndo wanapata nafasi ya kuambukizana, wanaoambukiza si wale wakimbiza mwenge, ni wanavijiji wenyewe kwa wenyewe wakitumia mkesha wa mwenge as an excuse

MN,

Si unaona research ya Mwanakijiji inachagua wrong sample. Itabidi aianze upya kama anataka kupata ukweli mzima!
 
Na jukwaa lilikuwa hivi:

Hivi hizi mbio za mwenge ni za CCM tu au ni za kitaifa?
Maana hapa naona chama kinaonyesha kwamba mbio hizi ni za chama fulani tu, na wanachama fulani hawana haki yakuwepo!

Au serikali ikichukuliwa na wapinzani basi mbio za mwenge ndio zitakua tamati?
 
Kwanza haya mambo ya research kwenye ukimwi nimekumbuka Mwakipesile alivyoshushuliwa juzi na JK. Alipokuwa anatoa hali ya ukimwi Mbeya akasema rate ya maambukizo imepungua hadi asilimia 3. Hii ilimshitua muungwana akahoji sana, mpaka akamwita mganga mkuu wa mkoa aeleze wametumia miujiza gani kufanikisha kushuka kwa rate ya maambukizi namna hiyo!
Eti yule mganga akasema walifanya utafirti wa nyumba kwa nyuma. Kikwete aliwashushua hapohapo akawaambia hiyo research yao ni fake na wafanye kazi upya
 
inaonyesha ni mbio za CCM, sijui CCM inatumia kiasi gani cha pesa kufanikisha mbio za mwenge na sherehe za kuuwasha na kuuzima? na pesa hizo wanazipata wapi?
 
..Mkuu najaribu kupekua pekua nijue price range ya huu mtambo....Nadhani muungwana nae amekuja na style mpya ya usafiri anaotaka kutumia......Bado kuna shule Kigoma wanafunzi wanakaa sakafuni hakuna madawati wao wanatukoga tu na migari yao.....

Mkuu Kipanga, hivi Rais wetu akitumia gari kama 504 ndio Wanafunzi wote Tanzania hawatakaa sakafuni? (Yaani shule zote za msingi zitakuwa zimepata madawati?)

Kama mtangulizi wake hakuwa na gari/magari kama hayo, je wanafunzi wote walikaa madawatini badala ya sakafuni?

Asante.
 
Mkuu Darwin,
CCM ndio Chama Tawala
Baadhi ya Vyama maarufu vya upinzani vinasema "Tukiingia madarakani tutafuta mbio za mwenge"
Mtikila mwenyewe miaka ya '90 alisema akipata madaraka atautupa mwenge baharini.

Najua kwa uhakika kwamba wote waliohudhuria kwenye hizo sherehe hawakua CCM bali watanzania, na neno watanzania linajumuisha kila itikadi, sasa iweje mwenge uwekewe bango la CCM.

Imekua nyakati nyingi kiongozi wa nchi waziri mkuu, sijui nani akitembelea sehemu fulani . kichwa cha habari kawatembelea wananchi wa wilaya au mkoa fulani lakini utaona nafasi hio wanaitumia kama chama baada ya kuitumia kitaifa.

Rais wa Tanzania ni rais pia wa wanachama wenye itikadi nyingine.
Waziri wa Tanzania ni wa wanachama wenye itikadi nyingine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…