Sherehe za miaka 60 ya Uhuru, Temeke mmejipangaje?

Sherehe za miaka 60 ya Uhuru, Temeke mmejipangaje?

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,430
Naandika haya nikiwa napita jirani kabisa na uwanja wa Uhuru (Uwanja wa Taifa), naona vikosi vya ulinzi na usalama vikijtaarisha kuanza mazoezi ya gwaride na mambo mengine, vijana wa halaiki nao hawajaachwa nyuma, naona kundi kubwa linaingia.

Ama kwa hakika kwa maataarisho haya, tutegemee shamra shamra na harakati kubwa siku ikifika, twende kwenye hoja sasa!

Nategemea katika kilele cha sherehe hizi, tarehe 9 Dec, 2021 tutapokea wageni wengi sana, wahadhi mbali mbali kutonga ndani ya nchi na nje ya nchi, kinachonisikitisha sasa, hadi naandika uzi huu bado siku 6 tuu na hakuna mataarisho yoyote ya miundo mbinu ya kuingia na kutokea.

Barabara za kuinglia na kutokea hapo uwanjani zipo ktk hali mbaya sana, swali langu je hii sherehe hamkujua kama itafanyika nyumbani kwenu?

Je, nini lifanyike ktk siku hizi zilizobaki ili kuweza kurekebisha hizo barabara?

"Naiona aibu mbele yangu"
 
Wale 'Makomandoo' waliopo katika Kesi ya Freeman Mbowe nao watakuwepo katika Maonyesho yao ili watuonyeshe 'Kiukakamavu' jinsi walivyokuwa 'Wakiteswa' na Polisi walivyokuwa rumande?
 
Back
Top Bottom