Sherekea vitu vidogo kuelekea vitu vikubwa

Sherekea vitu vidogo kuelekea vitu vikubwa

MIRA01

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2023
Posts
319
Reaction score
695
Idadi kubwa ya watu haswa jamii yangu ya kitanzania imekubwa na tatizo sugu la msongo wa mawazo.
Tatizo hilo limekuwa sugu kiasi kwamba watu wengi huishia katika maamuzi mabaya na hata wachache wao kuishia kuyatoa maisha yao.

Kuna mambo machache nimekuja kujifunza na hii mara baada tu nilipopunguza mwendo kuyafikiria maisha yenye kuogofya ya mambo ya jayo.

Nimekuja kutambua na kuelewa kuna haja sana kwa watu wengi ulimwenguni kuanza utamaduni mpya wa kusherekea ushindi ama mafanikia wanayoyapata maishani mwao,

Hii simaanishi ukaanza kufanya sherehe kubwa pale ambapo umevuta lengo la maisha yako! La hasha, wengi wetu tuna mambo kadhaa ambayo tumejiwekea na mengi huwa tunayafikia lakini kwa sababu hatuna utamaduni wa kujipongeza kesho yake hupanga malengo mapya nakuanza kukimbizana nayo usiku na mchana!

Badala yake tunashindwa kuelewa madhumuni maalamu ambayo yametufanya tuwepo ulimwenguni

Sasa basi rahi yangu ni hii, ni vyema kama umetimiza lengo lako hata liwe dogo kiasi gani basi usiache kulifurahia kamwe, lisherehekee kwa namna yoyote ile sio lazima uingie gharama kubwa kufanya hivyo!

Mfano, umepata elimu, sherekea, umepata ajira furahia na jamaa zako! Umeweza kulipa bills kama ada na kodi baada ya kufanya hvyo jipongeze kwa namna yoyote ile,

Hii inasaidia nini maishani mwako?
1. Itasaidia kuushawishi ubongo wako upambane kwenye malengo mapya uliyojiwekea na kuyakamilisha, tabia mojawapo za ubongo wa mwanadamu unafurahia zaidi sherehe kuliko huzuni. Hivyo ubongo utanya kitu kurudisha furaha.

2. Hupunguza msongano wa mawazo! Hii inatokea pale ambapo huoni hata ulichofanikisha kina dhamn ya kukifurahia sasa inakupelekea kuwa na msongo wa mawazo

Note: usipende kabisa kufananisha mafanikio yako na watu wengine! Kimbia mbio zako! Weka malengo yako yatimize kwa uwezo wako! Usife moyo kuona mwengine amefanikiwa zaidi yako
 
Tuurudi kwenye mada jua na dunia kipi kikubwa na kipi kinazunguka chenzake
 
Back
Top Bottom