Sheria 212 zatafsiriwa kwa Kiswahili, unadhani hii itasaidia wakati wa kesi hasa kwa Watanzania?

Sheria 212 zatafsiriwa kwa Kiswahili, unadhani hii itasaidia wakati wa kesi hasa kwa Watanzania?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Ndumbaro.jpg

Nimesoma hii habari kutoka Bungeni, kabla sijazungumza ninachotaka kuzungumza, isome kwanza wewe mwenyewe uone....

****
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema Sheria 212 kati ya sheria 466 zilizopo hapa nchini, zimetafsiriwa kutoka kwenye Lugha ya Kiingereza kwenda kwenye lugha ya kiswahili.

Amesema lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anazifahamu, kuzitii na kuzitekeleza sheria hizo

Waziri Ndumbaro ameyasema hayo, Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za Wabunge waliochangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo ikiwemo hoja ya utoaji wa elimu kwa Wananchi juu ya matumizi ya haki zao kwenye katiba na sheria za nchi, hoja iliyotolewa na mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo.

"Serikali kupitia wizara ya katiba na sheria imejipanga kila Mtanzania aweze kuelewa sheria, kutekeleza sheria na kuzitii sheria, ili suala la kutojua sheria lisiwe la utetezi na liweze kuondoka kabisa," alifafanua Dkt. Ndumbaro.

Aliendelea kusema kuwa, katika kuhakikisha kila Mtanzania anazifahamu, kuzitii na kuzitekeleza sheria, wizara imejikita kutafsiri sheria kwenye lugha ya Kiswahili.

*****

Hivyo basi ukifuatilia kesi nyingi Mahakamani ni ukweli kuwa watuhumiwa wengi huwa wanashindwa kujitetea au kuwa na msaada mkubwa kwa kuwa kuna maamuzi mengi yanafanywa kwa English.

Unakuta inaweza kutolewa hukumu, mtu unashindwa unalazimika kujichanganya kwa mawakili ambao wakati mwingine pamoja na sheria kuwa kichwani mwao lakini wanawez kushindwa kuwasilisha 1000% kile ambacho unaona kinatakiwa kuwasilishwa, kwa kuwa tu lugha inaweza kuwa mtihani.

Binafsi nadhani ni uamuzi sahihi, wewe unaonaje huu uamuzi wa kubadilisha sheria kuwa katika Lugha ya Kiswahili?
 
Utalii mpaka Sheria?
ndio eneo lake kitaaluma na alikuwa mwalimu ktk taaluma hiyo huku akiwa mkurugenzi kama sio mtendaji mkuu wa tazara...

alikuwa mwanasheria wa wachezaji kadhaa nchini na alishinda kesi nyingi kisheria , kabla ya tff kumuona mwiba mchungu ktk mambo yao ya mpira na kumpa lungu la kifungo cha soka

baada ya hapo magu akamuona... na yaliyo baki mnajionea
 
Back
Top Bottom