Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Unapokuwa na kampani ya watu katika mazungumzo yenu,endapo utapigiwa simu basi usiongee na simu kwa mda mrefu
Unapoenda kumtembelea mtu, baada ya kitambo kidogo ukisikia mwenyeji wako anasema anajisikia kuchoka, basi ujiongeze mda wa kuondoka umefika
Mtoto mdogo anapokuonyesha kitu basi onyesha kushangaa na kufurahishwa nacho, ina mpa furaha sana
Mtu anapo kuonyesha picha katika simu yake, basi usiswap kulia na kushoto kuangalia picha nyingine
Ukiazima gari la mtu basi kabla hujarirudisha hakikisha umelijaza full tank
Usijipige selfie mbele za watu, inawafanya watu wanao kuangalia kujisikia aibu kuona jinsi unavyohangaika sura ikae vizuri
Usimuombe mtu kitu ambacho unajua kabisa ndio hicho alichobakiwa nacho
Ni hayo tu!