Sheria gani na kanuni gani zimetungwa kipindi cha Magufuli zinatakiwa kutenguliwa?

Sheria gani na kanuni gani zimetungwa kipindi cha Magufuli zinatakiwa kutenguliwa?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Mi binafsi napenda ile sheria ya kutaka mtu anayefungua akounti youtube alipie. Au yule anayefungua blog, online tv na websites alipie. Tena kulipia pesa ndefu.

Ungependa kanuni na sheria gani kandamizi iondolewe?
 
Ile kanuni kuu kuliko zote iliyotungwa na kuingia kwenye damu za waTz kuwa ukiwa maskini na mnyonge basi wewe ndio mzalendo wa kweli na wewe ndio mwenye nchi. Kinyume chake wewe ni adui
 
Mi binafsi napenda ile sheria ya kutaka mtu anayefungua akounti youtube alipie. Au yule anayefungua blog, online tv na websites alipie. Tena kulipia pesa ndefu.

Ungependa kanuni na sheria gani kandamizi iondolewe?
1. Media service act ya 2016
2. Postal and electonic ( content) communication act 2018
3. Political parties act 2019
4. Money laundering and economic Sabortage Act.

5. Statistics Act.

Hizi zote zilitungwa sio kulinda maslahi ya nchi bali kulinda maslahi ya Jpm na genge lake la ndani ya ccm. Zililenga mahususi wapinzani ndani na nje ya chama chake.
 
Mi binafsi napenda ile sheria ya kutaka mtu anayefungua akounti youtube alipie. Au yule anayefungua blog, online tv na websites alipie. Tena kulipia pesa ndefu.

Ungependa kanuni na sheria gani kandamizi iondolewe?
Naunga mkono hoja!

Sheria ya kuthibiti watu kufungua channels zao youtube imesababisha content kutoka Tanzania kushare na Ulimwengu kuwa ndogo sana, Hii itaathiri hata vizazi vijavyo kushindwa kupata video content za maisha ya wananchi ya nyuma.

Imagine tuna vijana wana vipaji vya kuimba, kucheza soka, kuruka sarakasi, kusolve mahesabu na masomo mbalimbali, au skills fulanifulani wangependa kushare na dunia kama ambavyo dunia inashare nao lakini cha ajabu wanakutana na sheria isiyo rafiki inawathibiti

pia blog na Online ni chanzo cha ajira, kudhibitidhibiti hivi vitu ni kufunga ubunifu wa watu kutumia internet kujiletea kipato.

Tunaiomba serikali ya SSH iliangalie hili suala la kudhibiti watu kuwa na channels zao youtube na kumiliki blogs, iondoe ada zote na wananchi wawe hure online
 
Back
Top Bottom