Kisheria hakuna ndoa kati yenu ila kuna kitu kinachoitwa dhana ya ndoa. Ili dhana ya ndoa iweze kutimia yafuatayo lazima yathibitishwe
1. Nyie si maharimu
2. Jamii inayowazunguka inawatambu kuwa ni mume na mke
3. Mmeishi pamoja si chini ya miaka 2
4. Hakuna ndoa inayoendelea kati yenu
5. Wote wawili wamekusudia kuishi pamoja kwa kaisha yao yote.
Kuhusu malezi yawatoto anayepaswa kulea ni baba naiwapo watoto ni wadogo sana(chini ya miaka 7) basi watakaa kwa mama. Kwa kirefu zaidi tafuta sheria ya ndoa na soma kif cha 135,134, 133, na 125. Hapa utaelewa vizuri zaidi