Nashukuru sana kwa Mawazo yote yaliyotolewa!Kuhusu kuwaona Walimu baba yake alikwisha waona na infact aliitwa plae shuleni na kuelezwa hayo yote ambayo yameelezwa zuri zaidi hii ni mara ya pili kwa Walimu kufanya hivyo!Bwana mdogo alikwisha enda hadi USTAWI WA JAMII na kueleza matatizo ya mtoto kwa mama yake yapata miaka miwiliiliyopita na USTAWI walitoa Ushauri ya kuwa mama hana uwezo wa kumzuia mtoto kutoenda kwa baba yake ni suala la makubaliano na mwisho iliamriwa kuwa kwa vile mtoto alikuwa mdogo basi mama akae nae lakini inapofika Ijumaaa mtoto aende kwa baba yake hadi jumapili jioni kisha arudishwe kitu ambacho kilikuwa kinafanyika,ispokuwa toka mtoto aingie darasa la nne Mama amekuwa hataki mtoto aende kwa baba yake na badala yake inapofika Ijumaa huwa anatoa amri arudi kwake na ikifika jioni yeye humchukua na kumpeleka kwa rafiki zake hadi jpili usiku ambako hurudi kwa ajili ya shule jumatatu.
Tatizo tunaloliona ni maandalizi ya hovyo kimasomo kwa hali ya kawaida shule hizi za ENGLISH MEDIUM kama mtoto hasimamiwi vema zinaonekana kuwa ni ngumu kupita kiasi maana mambo mengine yanayo fundishwa mimi nilisoma nikiwa secondary school.
HATA HIVYO tunaangalia ushauri wowote tunaopewa kwa makini sana hasa hawa watu wa USTAWI ambao wametoa maagizo ya kuitwa baba na mama tarehe 16th Mwezi huu waangalie jinsi ya kuweka utaratibu sawa.Nawashukuru na tunasubiri Mawazo yenu.