Sheria inasemaje baba anapotaka kuchukua mtoto aliyezaa na mwanamke ambae hajaoana nae?

mtoto anayezaliwa nje ya ndoa au illegitimate child kisheria hatambuliki wala hana haki ya kurithi endapo utakufa ghafla bila kuacha usia jambo ambalo wato wengi hawajui ,lakini once you wiil legalize him or her she will be recognize legally na atakuwa na haki zote kisheria kama m,toto wako wa halali au wa ndoa so kuhalalishwa ndo kulegalize na hiyo ni baada ya mama mwenye mtoto kukubali.ukeeni manake ni upande wa mwanamke au mama
 
sheria ipo wazi mtoto kuwa chini ya mama akiwa u7,ila kama mama haeleweji baba anaweza mchukua akiweza kuwasilisha hoja vizuri mahakamani,sasa kama mtoto ni 8 old yrs jamaa akienda mahakamani ana shinda kesi chamsingi inabidi aka mhalalishe kwanza
 


Kwa nini hukuyaweka haya maelezo kwenye post yako ya kwanza? Kumbe tayari alishakwenda kwa ustawi wa jamii na wakakubaliana? Inaelekea kilichotekea sasa ni mwanamke kuvunja makubaliano. Ila fafanua hapo kwenye red. Kulikuwa na makubaliano kati yao au Ustawi wa jamii walitoa amri? Kama yalikuwa makubaliano ina maana mwanamke ameyavunja. Kama ilikuwa ni amri, then atakuwa amekaidi amri. Tofauti ni kwamba kukaidi amri inaweza kuwa na serious consequences zaidi. Badala ya kwenda kwa wanasheria, aende kwanza ustawi wa jamii hiyo tarehe 16, na aeleze exactly what is going on.
 
Vyovyote iwavyo...huyu mtoto anatakiwa kuendelezwa kielimu ili kumjengea maisha bora baadae...hivyo tafuteni ufumbuzi wa haraka ikiwa ni pamoja na hilo la kisheria ambalo lengo liwe kumsaidia mtoto na si kumkomoa mama yake! Km ulivyoeleza hukuongeza lako basi huyu dada anaweza kua na tatizo la kisaikolojia ambalo linahitaji kufanyiwa kazi!
 
Thanks tunashukuru na tunaendelea fanyia kazi hayo yote,Mawazo yenu yana mchango mkubwa kwa wote BABA,MAMA na MTOTO.
 

Hapo tatizo ni kwamba mtoto akichukuliwa huyo mama ataishi vp? wakati misaada inamiminika kwa ajili ya uwepo wa mtoto.
Kateni mirija ya misaada muone akiwashtaki hapo ndo pakumpatia mtoto.
 
Kuna kizungumkuti hapa.
Unasema mama ana kazi na aliwahi kwenda ulaya. Kwa nini hathamini elimu ya mtoto! kwa nini hathamini afya ya mtoto!
Fanya kila linalowezekana mkapime DNA kwanza.
Je huyo mama ameolewa? Je ana watoto wengine?
Je ni matunzo kiasi gani unatoa kila mwezi?
Majibu yatatupa uelekeo wa namna ya kukusaidia
 
Huyu Mama bado hajaolewa na hana mtoto mwingine,kwa ujumla matunzo ya kawaida kwa mwezi ni kati laki moja hadi laki ishirini achilia mbali
school fees na utilities zingine,kuhusu DNA tunaona haina haja kwa sababu mama mtoto hajawahi sema Mtoto si wa bwana mdogo,halafu bahati
nzuri au mbaya huyu mtoto huwezi uliza baba yake nani kwani ni photocopy ya Babake kabisa,tunashawishika kuwa hakuna shaka hata kidgo kuhusu huyo mtoto na baba yake.
Baba anatabia ya kula kucha-Mtoto naye hivyohivyo;
Baba anatabia ya kupenda sana kula nyanya -Mwana naye ni hivyohivyo
Baba na Mtoto wakikaa ni kama wachina ni copyright kabisa
Kama ikibidi DNA Test baba yuko tayri hata kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…