Sheria inasemaje juu ya hili

Sheria inasemaje juu ya hili

TUTEER

Senior Member
Joined
Nov 6, 2013
Posts
161
Reaction score
33
Mimi ni mwalimu wa shule ya sekondari, niliomba ruhusa kwa mkuu wangu kwa njia ya simu kwani shule ilkuwa imefungwa. Nilikaa muda wa wiki 1 lakini kabla ya kurudi shule nliambiwa ile nyumba niliyokuwa nakaa manager wa shule amefungua na kufanya ukarabat kwan wanajua nmetoroka. Pia wamefungia vitu vyangu.

Ndugu naomba msaada wenu sheria inasemaje, pia kama watakataa kunirudisha kazini nifanyaje?
 
Mi sijui sheria, ila walao najua kufagia vitu vya mtu bila ufahamu wake sio jinai. Hiyo inaangukia kwenye law of tort. Naomba wanasheria waje waendeleze kutokea hapo.
 
Hicho kitendo kinaangukia kwenye sheria nyingi tofauti. Unaweza kutumia penal code kwa kuwa amevunja/kuingia bila taarifa au ruhusa. Hii itakua jinai. Unaweza pia kutumia madai(civil) kwa trespass kwenye nyumba yako na mali
 
Mi naona ni madai under law of tort kwa vile motive ya mtu aliefagia nyumba iko wazi. Ni kwamba kwa kuwa mlalamikaji alikosekana kwenye nyumba aliyopewa kwa offer kwa muda bila taarifa, mmiliki akaamua kutumia haki yake ya umiliki kufagia, kwa kufagia kila kitu mmiliki hana kosa. Under law of tort mmiliki atajibu kesi kwanini hakujiridhisha kuwa aliyepewa nyumba ameondoka kweli au la. Hapaswi kutenda kwa kukisia. Jambo la pili mlalamikaji hajaeleza hali ya vitu vilivyofagiliwa. Je alivikuta vimetunzwa mahali salama au viliharibiwa. Kama vimeharibiwa, atapaswa kufungua jinai under penal code.
 
Kwangu mimi hapo naona kuna makosa kama mawili au matatu,
(1) Tresspas to goods lied under the lwa of tort,
(2) House breaking under penal code section 296, CAP 16 R.E 2002
(3) Unlawfully detains of good.
Kwahio ndugu unaweza kushtaki kwa magosa kama hayo hapo kosa la jinai na pia madai asante.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mim ni mwl wa shule ya sec,nliomba ruhus kwa mkuu wang kwa njia ya cm kwan shule ilkuwa imefngwa
Kwa kuanzia, serikali haifanyi kazi kwa njia ya simu, bali njia hiyo inaweza kutumika kutoa tuu taarifa ya awali, lakini taarifa yoyote rasmi, hufanywa kwa maandishi!.

Hata wakati shule imefungwa, ofisi ya shule ya kupokea barua yako ya ombi la ruhusa huwa iko wazi!.

Mfanyakazi yoyote wa umma, atapopata tatizo, anatoa taarifa rasmi kuomba ruhusa, akiishakubaliwa ndipo huondoka na sio kutangulia kuondoka ndipo anatuma taarifa kwa simu!.

Ulipoajiriwa naamini ulipewa barua unayokueleza kila kitu, ila kwa waalimu wapya, "absconding" ni tatizo sugu, hivyo mwalimu anapokuwa hajaonekana for lets say 7 days na hakuna taarifa yoyote rasmi, Mkuu wa shule yuko righ kukuhesabu ume abscond, hivyo sasa ni jukumu lako to prove your case kuwa sio abscondment case, utasikilizwa na utarejeshwa kazini!.

Kwa ushauri tuu, don't go into legal battle unless umeamua huitaki tena kazi hiyo ya ualimu, its time consuming, wastage of time and you'll end up getting nothing hata kimahakama ukishinda na kutakiwa kufidiwa!.

Japo haki ni jambo la msingi kabisa, lakini haki hiyo unayoitafuta iwe na maana kwako unless wewe ni wale wako tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku!
Pasco
 
Mim ni mwl wa shule ya sec,nliomba ruhus kwa mkuu wang kwa njia ya cm kwan shule ilkuwa imefngwa,nlikaa mda wa wk 1 lakn kabla ya kurdi shule nliambiwa ile nyumba nliyokuw nakaa manager wa shule amefngua na kufanya ukarabat kwan wanajua nmetoroka!,pia wamefngia vi2 vyang,ndg naomba msaada wenu sheria inasemaje,pia kama watakataa kunrudisha kazn nfanyaje?

Mwalimu gani unashindwa kunyosha maelezo...Trespassing is entering someone's property without permission or lawful excuse
 
Back
Top Bottom