Hivi majuzi tumeshudia picha chafu za bibi harusi kwenye mitandao mpaka ndoa yake kuvunjika ghafla baada ya fungate.Niliona jinsi swala la kule morogoro la kubakwa yule msichana watu walivojitokeza kwa wingi mpaka viongozi kulaani kitu hicho na hatimae kuwatia nguvuni wahusika.
Kitu najiuliza hivi hata kama msichana alipiga kwa ridhaa yake je ni sawa kwa EX wake kuzisambaza kiulaini hivo na sheria isichukue mkondo wake?Huyu jamaa anajulikana fika ni nani na yupo wapi lakini naona hata wale wa haki za wanawake wapo kimya, hivi bado tumepigwa mshangao au hii kitu inaruhusiwa tu so long ni pic za mpenzi wako wa zamani.
Mkuu kuna mambo mengi kwenye tukio hili, kuna makosa ya kijamii civil cases na kuna makosa ya jinai, criminal,
1. Kwanza ieleweke, kwa mujibu wa sheria za Tanzania, umri wa mtoto (minor) ni miaka 14!, hivyo kufanya mapenzi na yoyote, kwa ridhaa yake, baada ya umri wa miaka 14, sio kosa kisheria, hivyo mhusika wa picha zile, hakufanya kosa lolote kisheria kufanya aliyoyafanya.
2. Kuna aina za mapenzi zinazoruhusiwa kisheria, na kuna aina za mapenzi ambazo haziruhusiwi kimaadili, na kuna aina za mapenzi ni kinyume cha sheria, kufanya mapenzi kinyume cha maumbile, ni kinyume cha maadili na sii kinyume cha sheria, hivyo huyo dada/kaka kufanya mapenzi kinyeme cha maumbile kwa ridhaa yao wenyewe, hawajavunja sheria yoyote.
3. Kupiga picha zozote na mpenzi wako, hata kupiga picha chafu za aina gani, as long as mmezipiga kwa ridhaa yenu, sio kosa lolote la kisheria, bali ni kosa kimaadili, huyo dada hajafanya kosa lolote kisheria kupiga picha chafu.
4. Kuna kitu kinaitwa "the right to privacy" yaani haki ya faragha, hii ni haki ya mambo mtu anayoyafanya kwa faragha kubaki kuwa faragha, hivyo inapotokea watu mlikuwa kwenye faagha fulani, mkifanya mambo yenu faraghani, ikiwemo kupiga picha za utupu, hayo yote yanahesabika kuwa yamefanywa kwa faragha, ikitokea kuna mmoja wa wana faagha hao, amezitoa picha za faragha kwenye public, bila ridhaa ya mwana faragha mwenzake, ni kosa la kijamii linaloitwa "defamation" hivyo huyo dada anaweza kumfungulia kesi ya madai huyo ex wake kwa kitendo tuu cha kuzichapisha picha zao za faragha na kuzisambaza.
NB. Kwenye kesi hiyo, lazima ithibitishwe jee ni nani aliyezisambaza picha hizo, inawezekana kabisa, wapenzi mlipiga picha za mahaba kwa nia njema ya faragha, lakini picha hizo zikadondokea katika mikono isiyo salama na kusambazwa, kosa ni usambazaji!. Katika tukio husika hakuna popote palipoonyesha hizo picha zililetwa na nani, hivyo hakuna mtu wa kumshitaki!.
5. Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, picha zile zilitumwa privately kama parcel kwa maharusi, na zilibainika nyumbani kwa maharusi hao baada ya fungate!, ikumbukwe nyumba zote ni private na zina haki ya faragha, yaani kitendo cha kutoa mambo ya ndana ndani ya nyumba hizo, nazo zina maeneo ya faragha zake, mfano mambo yanayotokea chumbani kwenye nyumba hiyo hiyo ni faragha ya chumbani, hayapaswi kufika hata sebuleni, mambo ya chooni ni faagha ya chooni hayafai kufika sebuleni!, hivyo mzigo wa picha ulianzia chumbani, kwa hao walioziona humo chumbani, mambo yalipaswa kuishia humo humo chumbani!, sasa msambazaji mkubwa wa faragha ile ni aliyezitoa picha chumbani, hadi sebuleni, hadi nje ya nyumba, hadi mitandao ya jamii, na wahusika kwenda kwenye vituo vya edia kutangaza faragha zao!.
6. Ikithibitika ni nani aliyezisambaza kwenye mitandao ya kijamii, hapo ndipo jinai inapoanzia hapo na inawahusu wote waliozipokea na kuzisambaza!.
7. Ili kufungua kesi yoyote, hatua ya kwanza ni kumtafuta mhusika wa kosa husika, hapa kosa la madai, civil ni kusambaza picha za faragha kwenye public ya watu, na litamhusu aliyekuwa na hizo picha na kuzituma kwa maharusi!. Kosa la pili ni la jinai la kusambaza picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii na zitamhusi aliyeziingiza kwenye mitandao, na unaweza kukuta huko kote hata huyo ex wala hahusiki!.
My Take.
Huyu bwana harusi na mkewe ndio wahusika wakuu number moja kwa kutoa ndani mambo yao aibu zao za ndani na kuyamwaga hadharani, kama mtu unampenda kwa dhati mke wako, utamfichia aibu yake!, picha zile zingeishia pale pale chumbani!, jianaume zima linahojiwa redioni linaongea kwa uchungu utadhani lenyewe ndio lililokuwa la kwanza!. Kuna watu wameoa wanawake waliokuwa wakijiuza, na kwenye biashaa hiyo wameingiliwa kote hadi mande milango yote, na bado wamekuja kuwa wake wazuri kabisa kwenye ndoa zao!, kama pendo la dhati lipo, picha ndio nini?!.
Pasco