Dar_Millionaire
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 227
- 86
Wadau naomba ushauri.
Nyumba yangu ina ukuta na geti. Mtu hawezi kuingia bila kukaribishwa, labda awe mwizi. Nataka kutega umeme madirishani na mlangoni ili kama mwizi karuka ukuta akigusa tu dirisha au mlango apigwe shoti.
Umeme huo wa mtego utakuwa unawashwa mida ya usiku na mtu wa mwisho kulala. Takribani mida ya kuanzia saa tano usiku mpaka saa 12 alfajiri. Kama kuna mtu yuko macho ndani ya nyumba jukumu lake la kwanza ni kuzima mtego. Anawasha pale tu anapokuwa yeye ni mtu wa mwisho kulala.
Mchana hautawashwa hata kama hakuna mtu nyumbani. Hii ni kwa kuwa matukio ya wizi wa kuruka ukuta hapa mtaani yanatokeaga usiku tu.
Swali ni je katika mazingira kama haya ya nyumba yenye geti na ukuta je sheria inasemaje kuhusu kuweka mtego wa aina hii?
Ikitokea mwizi kajeruhiwa (au kafa) kwa shoti ya umeme je nitakuwa na kesi ya kujibu? Kama ndiyo, je kwa sheria ipi na kifungu kipi?
Je mwizi huyo anaweza kujitetea kwamba hakuja kuiba kwa kuwa atakuwa hajafanikiwa kuiba na hivyo hakuna ushahidi wa kwamba ni mwizi? Au kitendo cha kuruka ukuta tu kinatosha kumhukumu mtu kwamba ni mwizi (au mvamizi) hata kama hajaiba chochote.
Na je ni lazima niweke kibao cha "Tahadhari nyumba hii inalindwa na mtambo maalumu wa kuzuia wezi", au kwa kuwa mtego umo ndani ya fence hakuna ulazima?
Natanguliza shukrani.