Sheria Inasemaje Kuhusu Kutega Umeme Kuzuia Wezi

Sheria Inasemaje Kuhusu Kutega Umeme Kuzuia Wezi

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2008
Posts
227
Reaction score
86
Wadau naomba ushauri.

Nyumba yangu ina ukuta na geti. Mtu hawezi kuingia bila kukaribishwa, labda awe mwizi. Nataka kutega umeme madirishani na mlangoni ili kama mwizi karuka ukuta akigusa tu dirisha au mlango apigwe shoti.

Umeme huo wa mtego utakuwa unawashwa mida ya usiku na mtu wa mwisho kulala. Takribani mida ya kuanzia saa tano usiku mpaka saa 12 alfajiri. Kama kuna mtu yuko macho ndani ya nyumba jukumu lake la kwanza ni kuzima mtego. Anawasha pale tu anapokuwa yeye ni mtu wa mwisho kulala.

Mchana hautawashwa hata kama hakuna mtu nyumbani. Hii ni kwa kuwa matukio ya wizi wa kuruka ukuta hapa mtaani yanatokeaga usiku tu.

Swali ni je katika mazingira kama haya ya nyumba yenye geti na ukuta je sheria inasemaje kuhusu kuweka mtego wa aina hii?

Ikitokea mwizi kajeruhiwa (au kafa) kwa shoti ya umeme je nitakuwa na kesi ya kujibu? Kama ndiyo, je kwa sheria ipi na kifungu kipi?

Je mwizi huyo anaweza kujitetea kwamba hakuja kuiba kwa kuwa atakuwa hajafanikiwa kuiba na hivyo hakuna ushahidi wa kwamba ni mwizi? Au kitendo cha kuruka ukuta tu kinatosha kumhukumu mtu kwamba ni mwizi (au mvamizi) hata kama hajaiba chochote.

Na je ni lazima niweke kibao cha "Tahadhari nyumba hii inalindwa na mtambo maalumu wa kuzuia wezi", au kwa kuwa mtego umo ndani ya fence hakuna ulazima?

Natanguliza shukrani.
 
Miaka ya nyuma vifo va bahati mbaya vya wakazi wa nyumba zilizokuwa zimetegwa umeme madirishani na milangoni vilitokea, umakini unahutajika kuzuia hali hii isitokee. Sina hakika sheria inasemaje.
 
Sidhani kama inazuiliwa, unaweza kuweka tu ila lazima uweke viashiria kwa maandishi au alama kuwa kuna umeme ili mtu asome na kuona!!!
 
Wewe weka tu sharti uweke alama sehem ya kwamba nyumba hii ina mtambo wa kuzuia wizi kwa kutumia umeme usipoweka alama hiyo mwizi atakaye kamatwa au nduguze wanaweza kuku sue..!
 
zaidi viashiria itakubidi uviweke sehemu ambapo yeyote awaye mwizi na asiye aweze kuona na kuelewa kuwa kuna hali kama hiyo maeneo hayo.tofaui na hapo utashitakiwa bcoz utakuwa hujatake DUTY OF CARE TO TRESPASSERS.SOMA SHERIA YA MAKOSA YA JINAI CAP 16 RE 2002 Ss.233 to 234.
 
UTAFUNGWA KAKA......SISTER ALITEGA ILI KUZUIA WEZI WA KUKU.....AKASAHAU KUZIMA KITU AMBACHO KINAWEZA KUTOKEA,....akaua mtoto na sasa yupo jela
 
Dah! Hapo natatizika kidogo, mana kwa mtu kama mwizi ukimuwekea viashiria si obvious atatafuta altenatives zingine ili aweze kuingia na kama sheria ndio inasema ivo, hatuwezi pinga ila kuna umuhimu waku ireview ili ifanyiwe amendments. Mwizi hana haki ya kujua security system unayotumia. Ni mtazamo tu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom