Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009, Sheria namba 8 kuanzia ibara ya 45 hadi 47 inaeleza taratibu za upimaji wa vinasaba kwa mama mjamzito, kijusi na mimba iliyotungwa nje (extracorporeal embryos).
Vipimo vya vinasaba kwa mama mjamzito havitakiwi kufanyika ila pale tu vinapohitajika kwa ajili ya matibabu.
Vilevile, Mama Mjamzito ana haki na mamlaka juu ya sampuli ya vinasaba vya binadamu iliyochukuliwa kwake kwa lengo la matibabu.
Ukusanyaji wa sampuli ya vinasaba vya binadamu kutoka kwa kijusi kwa lengo la matibabu unatakiwa kufanyika kulingana na ushauri wa daktari wa matibabu. Endapo mtu atabainika kukusanya sampuli bila idhini ya daktari atakuwa ametenda kosa kisheria.