ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,753
- 9,575
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo maana nikaweka alama ya kuuliza nikiashiria kwamba kuachana kunawezekana kabisa kwa sababu hamjapigiliwa misumari licha ya mafundisho au matakwa ya baadhi ya imani za kidini kwamba hakuna kuachana mpaka kifo kiwatenganishe.
Nimeeleweka sasa?
acha hadithi zako za kizamani soma 1wakorintho 7:1 mlango wote ndipo utaelewa somo hapo juu
Maudhi katika ndoa yanaweza kuwa mazito sana na
ndipo mlalamikaji mume au mke anapokwenda
mahakamani kudai amri ya kuvunja ndoa kabisa
ambayo inaitwa amri ya talaka.
Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inasema ya kuwa
mashauri ya kudai talaka ambavo lazima yatolewe
na mahakama yanapaswa kwanza kupitia kwenye
baraza Ia usuluhishi. Mabaraza ya usuluhishi yapo
mengi na yameundwa kwa shughuli hiyo kwenye
vijiji na mijini. Jukumu Ia mabaraza hayo ni
kuwasuluhisha mlalamikaji na mlalamikiwa ili
waweze kusameheana. Baraza hilo linaposhindwa
kusuluhisha, hawana budi kutoa shahada kwa
mume na mke wanaohusika. Shahada
hiyo itamwezesha mlalamikaji kufungua
madai ya talaka kwenye mahakama. Bila
shahada hiyo madai hayawezi kupokele-
wa mahakamani. Sababu zinazoweza kuf-
anya ndoa ivunjike.
(a) Maasi au utoro wa makusudi
usiopungua miaka mitatu.
(b) Mlalamikiwa kufungwa jela kwa
muda wa miaka mitano mfululizo au
maisha.
(c) Kutengana kwa hiari au kwa amri ya
mahakama kusikopungua miaka
mitatu.
(d) Ukatili wa mwili au akili kwa watoto
wa ndoa au kwa mlalamikaji.
(e) Kichaa kinachothibishwa na
madaktari wawili kwamba hakiponi.
(f) Mlalamikaji kubadili dini ikiwa wote
walikuwa na dini moja wakati wa
kuoana.
Kwa mujibu wa dini hiyo kubadili dini
kunavunja ndoa au kunakuwa na sababu
za kuvunja ndoa
Ahsante Mentor kwa maelezo mafupi ya ufashaa...swali la nyongeza, kwenye kugawana mali zilizochumwa mikiwa kwenye ndoa, mgawanyo ukoje/ hasa inapokuwa mume ndio 'main bread winner' bila mchango wowote toka kwa mke, japo naye ana kazi na/au biashara ndogo ndogo.
Mali zina gawiwakulingana na mchnago wa mtu kwenye mali husika. kama huna mchango kwenye mali husika basi siyo haki yako. lakini kama ulimnunulia gari mkeo na ukampa kama zawadi hiyo itabaki ni mali yake.